UTURUKI
2 dk kusoma
Wanasayansi wa Kituruki waunda programu inayotumia sauti kutambua saratani ya mapafu mapema
Utafiti unaonyesha programu hugundua saratani ya mapafu mapema kwa usahihi wa zaidi ya 90%.
Wanasayansi wa Kituruki waunda programu inayotumia sauti kutambua saratani ya mapafu mapema
Programu inayotumia sauti ya kugundua saratani ya mapafu mapema / AA
29 Aprili 2025

Wanasayansi wa Uturuki wameunda programu-tumizi inayotumia akili mnemba iliyoundwa kugundua saratani ya mapafu mapema kwa kuchanganua sauti ya mtu.

Ikiongozwa na Dk. Haydar Ankishan kutoka Taasisi ya Stem Cell katika Chuo Kikuu cha Ankara, pamoja na michangio kutoka kwa wanasayansi katika taaluma nyingi, mradi huo unalenga utambuzi wa mapema wa saratani ya mapafu, ambayo mara nyingi hutambuliwa tu katika hatua zake za juu.

Akizungumza na waandishi wa habari, Ankishan alisema: "Katika utafiti wetu, tulizingatia muundo wa sauti, muuondo wa anatomiki ya mapafu, na mfumo wa mzunguko wa damu na kupendekeza kwamba sauti inaweza kutoa habari kuhusu saratani ya mapafu. Tulifuata wazo hili."

"Baada ya karibu mwaka mmoja na nusu wa kazi, tumepata matokeo mazuri," alisema.

"Tumegundua kwamba saratani ya mapafu, haswa katika hatua yake ya kwanza, inaweza kugunduliwa katika mapema kwa kiwango cha usahihi cha zaidi ya 90%," alisema.

Dk. Bulent Mustafa Yenigun, anayefundisha katika Shule ya Tiba ya Chuo Kikuu cha Ankara na ni mmoja wa timu hiyo ya utafiti, alisisitiza kuwa jambo muhimu zaidi katika kutibu saratani ya mapafu ni kuigundua mapema.

"Tulifanya utafiti wetu na kikundi kilichojumuisha wagonjwa 50 na watu 50 wenye afya njema," alisema.

"Mswada wa kuongea wa dakika mbili ulitayarishwa kwa kila mgonjwa kwa uchambuzi wa sauti, na sauti zao zilirekodiwa," alisema.

Akisisitiza kwamba rekodi zote zilifanyiwa uchambulizi katika hali sawa, alisema: "Programu yetu inagundua mabadiliko katika sauti na inatoa onyo kwamba kunaweza kuwa na saratani ya mapafu.

CHANZO:AA
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us