UTURUKI
1 dk kusoma
Uturuki inaunga mkono mazungumzo ya amani kati ya Urusi na Ukraine— Fidan
Kulingana na Hakan Fidan, Ankara inaunga mkono usuluhishi wa mgogoro kati ya Urusi na Ukraine, uliodumu kwa miaka mitatu.
Uturuki inaunga mkono mazungumzo ya amani kati ya Urusi na Ukraine— Fidan
Kulingana na Hakan Fidan, Ankara inaunga mkono usuluhishi wa mgogoro kati ya Urusi na Ukraine, uliodumu kwa miaka mitatu. / TRT World
21 Machi 2025

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan amesema kuwa Ankara itaunga mkono usuluhishi wa mgogoro kati ya Urusi na Ukraine, kama unavyosimamiwa na Marekani.

"Tunaunga mkono mazungumzo haya,"alisema Fidan katika mkutano na waandishi wa habari, akiwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Hungaria kwenye mji mkuu wa Ankara siku ya Ijumaa.

Kuhusu usalama wa Ulaya, Fidan alisema: "Tunaamini kuwa hatua zote za amani ya Ulaya, pamoja na Uturuki ni kwa ajili ya manufaa yetu wote."

"Ni mategemo yetu kuwa sera za Brussels hazitoyumbisha mazungumzo hayo ili kumaliza mgogoro huu, alisema Waziri wa Mambo ya Nje wa Hungaria Peter Szijjarto.

Kulingana na Szijjarto, suala la usalama wa Ulaya litakuwa halina maana yoyote bila ushirikishwaji wa Uturuki na Urusi.

Siku ya Jumanne, Rais wa Urusi Vladimir Putin alikubaliana na pendekezo la Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu Urusi na Ukraine kuacha kushambuliana, hasa kwenye miundombinu yao ya nishati kwa siku 30, kulingana na taarifa iliyotolewa na Kremlin.

CHANZO:TRT World
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us