AFRIKA
2 dk kusoma
Kenya yashawishi wananchi kununua nyumba za serikali
Kwa sasa nyumba 4, 888 ziko tayari kununuliwa kwa ajili ya makazi.
Kenya yashawishi wananchi kununua nyumba za serikali
Rais Willim Ruto amevumbua mradi wenye lengo la kujenga nyumba 200,000 kila mwaka/ picha/@bomayangu / Public domain
28 Aprili 2025

Serikali ya Kenya inawahimiza wananchi kununua nyumba ambazo imejenga chini ya mradi wa Rais William Ruto maarufu kama "Boma langu.”

Rais Ruto amesema mradi huo una lengo la kutoa makazi ya gharama nafuu kwa Wakenya wa tabaka mbali mbali huku akilenga kujenga nyumba laki mbili kila mwaka.

Ni mradi ambao awali umepingwa na baadhi ya wananchi wanaosema kuwa si haki kwa serikali kuwakata fedha kwa lazima kwa lengo la mradi huo, na baadae kuwauzia.

Tozo ya lazima

Rais wa Kenya William Ruto, 19 Machi 2024 aliidhinisha sheria ya Makazi ya bei nafuu, 2024, ambayo iilikuwa na athari za papo hapo kwa waajiri.

Hii ilikuwa baada ya utekelezaji wake kusimamishwa na Mahakama Kuu ya Kenya kwa masharti ya kukatwa na kutuma kwa ushuru wa nyumba kama ilivyoanzishwa kupitia Sheria ya Fedha, 2023.

kwa sasa Mwajiri anatakiwa kutuma kwa kila mfanyakazi mchango wa 1.5% ya mshahara wa kila mwezi wa mfanyakazi na mchango wa mfanyakazi kwa 1.5% ya mshahara wa kila mwezi wa mfanyakazi.

Masharti ya kukatwa na kutumwa kwa ushuru yalianza kutumika tarehe iliyoidhinishwa.

Sheria inasema adhabu ya 3% kwa kiasi ambacho hakijalipwa itatozwa kwa watu ambao watashindwa kuwasilisha ushuru kwa tarehe inayotarajiwa.

Miradi inaendelea

Serikali inasema ina miradi kumi ya ujenzi wa makazi haya yamekamilika katika sehemu tofauti ya nchi , huku watu 45,00 wakiripotiwa tayari wamepata makazi yao.

Katika tovuti ya mradi huo inaonyesha kuwa zaidi ya watu 350,000 wamejisali kwa ajili ya kupata nyumba huku miradi mengine zaidi ya 40 ikiendelezwa.

Bei ya nyumba ni kati ya dola za Marekani 4,900 kwa nyumba ya chumba kimoja, dola 7,400 kwa ile yenye chumba kimoja cha kulala na dola 9,800 kwa ile ya vyumba viwili.


CHANZO:TRT Afrika and agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us