Serikali ya Ethiopia inasema kuwa mipango ya kuwapokonya na kuwarejesha katika jeshi na jamii waliokuwa wapiganaji katika vita vya Tigray Kaskazini mwa nchi umechelewa.
Mnamo Novemba 2022, serikali ya Ethiopia na Chama cha Tigray People’s Liberation Front chenye msingi wake kaskazini mwa nchi, (TPLF) walitia saini makubaliano ya amani yakumaliza mzozo wa miaka miwili ambao uliua maelfu na mamilioni ya watu kuhama makazi yao.
Mkataba wa Pretoria kama unavyoitwa unatoa wito wa kupokonywa silaha, kwa wapiganaji na kuunganishwa tena katika jamii na jeshi la taifa.
Kati wa wapiganaji waliolengwa 75,000 wa zamani kupitia mchakato wa Kupokonya Silaha, Uondoaji, na Kuwaunganisha tena (DDR) kufikia Juni, ni 17,000 pekee ndio wamekamilisha mchakato huo hadi sasa.
Temesgen Tilahun, Kamishna wa Tume inayohusika na hayo, NRC, aliviambia vyombo vya habari kuwa mpango huo, uliozinduliwa katikati ya Novemba 2024,“umechelewesha.”
Temesgen alielezea kuwa kukosekana kwa utulivu wa kisiasa katika eneo hilo "kumeleta kikwazo kikubwa," na kulazimisha Tume kusimamisha shughuli zake.
"Tulilazimika kusimamisha kazi yetu," alisema, akiongeza kuwa "kulikuwa na masuala ambayo tulihitaji kuyafafanua," ikiwa ni pamoja na uchunguzi wa taarifa za wapiganaji wa zamani na "shirika na makabidhiano ya silaha."
Kulingana na Temesgen, hadi wakati shughuli zilipositishwa mwishoni mwa mwezi Disemba 2024, ni takriban 8,000 wa zamani tu waliokuwa wamekamilisha ukarabati na uondoaji.