Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amefanya mazungumzo na Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud ,katika Ikulu ya Rais, jijini Ankara siku ya Alhamisi.
Wakati wa kikao hicho, nchi hizo zilijadiliana masuala mbalimbali, yakiwemo ya kiushirikiano, huku Rais Erdogan akisisitiza kuwa Uturuki inatoa kipaumbele kwenye suala la amani, utulivu na heshima ya Somalia, akisisitiza kuwa mchakato wa kutafuta suluhu kati ya Somalia na Ethiopia bado unaendelea.
Kulingana na Rais Erdogan, ushirikiano na Somalia katika kupambana na ugaidi utaendelea, na kuongeza kuwa Uturuki bado iko upande wa Somalia katika mapambano hayo.
Katika kikao hicho, Rais Erdogan alisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Uturuki na Somalia katika nyanja za kiuchumi, biashara, ulinzi na usalama.