logo
swahili
Moshi mweusi siku ya pili ya uchaguzi wa papa

Moshi mweusi umeonekana katika paa la kanisa la Sistine, Vatican baada ya makadinali kuingia katika siku ya pili ya kumchagua Papa wa Kanisa Katoliki. Hii inaashiria kuwa makadinali hao 133 bado hawajampata kiongozi mpya wa kanisa hilo. Matangazo mengine matatu yanatarajiwa Alhamisi.

Moshi mweusi siku ya pili ya uchaguzi wa papa
Wakusanyika siku ya pili wakisubiri matokeo ya uchaguzi wa Papa

Waumini wa Kanisa Katoliki na watu wengine wamekita kambi Vatican wakisubiri matokeo ya Alhamisi ya kumchagua papa mpya.Jumatano moshi mweusi ulionekana kuashiria hakukuwa na papa aliyechagualia.Leo moshi unatarajiwa kuonekana mara nne.

Wakusanyika siku ya pili wakisubiri matokeo ya uchaguzi wa Papa
Mchakato wa kumchagua papa waingia duru ya pili Mei 8

Makadinali 133 wa Kanisa Katoliki leo Mei 8, wanaingia katika duru ya pili ya upigaji kura wa papa mpya. Waumini wa Kanisa hilo duniani wanasubiri kwa hamu kuona moshi mweupe ambao ndio utaoashiria kupatikana kwa kiongozi mpya wa kanisa.
Mchakato huo, ulioanza Mei 7, ulitoa moshi mweusi, ukiwa na maana kwamba, bado papa mpya hajapatikana.

Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us