AFRIKA
2 dk kusoma
Uturuki inatoa wito kwa pande zote Libya kuanza majadiliano ya kutafuta suluhu
Wizara ya Mambo ya Nje imeeleza kuwa Uturuki iko tayari kutoa mchango wake katika kuhakikisha ‘kunapatikana suluhu endelevu na ya kudumu kwa mzozo huo’
Uturuki inatoa wito kwa pande zote Libya kuanza majadiliano ya kutafuta suluhu
Gari la jeshi likionekana badaa ya kuchomwa moto katika mapigano kati ya vikosi vya Libya na wapiganaji wa ‘’Stability Support Apparatus’’ kufuatia kusitishwa kwa mapigano katika mji mkuu wa Libya, Tripoli 14 Mei, 2025
14 Mei 2025

Siku ya Jumatano Uturuki imetoa wito kwa pande zote nchini Libya kufanya majadiliano ya kutatua matatizo yao pamoja na kusitisha mapigano

"Tunatoa wito kwa pande zote kutekeleza kikamilifu usitishwaji wa mapigano bila kuchelewa na kufanya majadiliano ya kutatua mzozo," ilisema taarifa hiyo ya Wizara ya Mambo ya Nje.

Taarifa hiyo imekuja baada ya vurugu kuzuka kati ya makundi yenye silaha katika maeneo mbalimbali ya mji mkuu Tripoli.

Uturuki "inafuatilia kwa karibu’’ hali tete iliyopo ndani na karibu na Tripoli, iliongeza.

Taarifa hiyo pia ilieleza utayari wa Uturuki kuchangia katika kupatikana kwa suluhu ya kudumu na endelevu katika nchi hiyo.

Wizara ya Ulinzi ya Libya ilisema siku ya Jumatano kuwa mapigano yalisitishwa baada ya machafuko hayo ya makundi yenye silaha.

Taarifa ya wizara hiyo ilisema kuwa mapigano yalisitishwa katika maeneo yote mjini Tripoli kama sehemu ya juhudi hizo “ili kulinda raia, kulinda taasisi za serikali, na kuepuka mapigano zaidi.”

Inasema vikosi vya usalama, vikishirikiana na mashirika mengine ya usalama, wamechukua hatua zinazostahiki kurejesha hali ya utulivu, ikiwemo “kupelekwa kwa vikosi visivyoegemea upande wowote kuhakikisha kuna utulivu na kuepuka mzozano zaidi."

Wizara hiyo imetoa wito kwa pande zote kutimiza ahadi ya kusitisha mapigano na kujiepusha na hatua zozote ambazo zitasababisha kuanza tena kwa mapigano.


CHANZO:AA
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us