Malkia Amina: Mwanamke shupavu na jasiri kutoka Zazzau nchini Nigeria
Malkia Amina: Mwanamke shupavu na jasiri kutoka Zazzau nchini Nigeria
Akiwa shujaa na mwanamkakati wa kweli, Malkia Amina wa Zazzau amepambana na vikwazo mbalimbali na kuacha urithi usiofutika katika karne ya 16.
14 Mei 2025

Miaka mingi kabla dunia haijaanza kufumbata mijadala ya kijinsia, eneo la Afrika Magharibi lilisifika kwa kuwa na himaya zenye nguvu na mila na desturi imara.

Kipindi hicho, utawala ulikuwa chini ya milki ya mwanaume, kabla ya ujio wa Malkia Amina kutoka dola ya Kihausa, iliyokuwa ikujulikana kama Zazzau.

Mwanamama huyu alisifika kwa kutumia busara wakati wa utawala wake.

Akiwa amezaliwa na Mfalme Nikatau na Malkia Bakwa Turunku, Amina aligoma kukubaliana na majukumu waliyokuwa wakipewa wanawake wakiwa wangali wadogo.

Aliandaliwa na babu yake kupigana na kijeshi wakati mabinti wa rika lake walipokuwa wakusubiria kupangiwa majukumu mengine ya kijamii.

Alipofikisha miaka 16, Amina alipewa jina la “Magajiya”, lenye maana ya mrithi.

“Kuna simulizi tofauti kuhusu maisha ya Malkia Amina wa Zazzau. Kinachokubalika zaidi ni kuwa alikuwa moja ya mabinti wa Bakwa Turunku, aliyeitawala Zazzau katika karne ya 16,” anasema Profesa Ibrahim Malumfashi, mtaalamu wa historia ya fasihi ya kihausa kutoka Chuo Kikuu cha Jimbo la Kaduna, katika mahojiano yake na TRT Afrika.

“Asili yake ni kwenye mji wa kale wa Turunku, ulio kilomita chache kutoka Zaria.”

Malkia Zazzau anakumbukwa kwa udhibiti wake wa eneo la Zaria kwa kujenga ukuta wa Ganuwa.

Kama hiyo haitoshi, Malkia Zazzau, alianza kampeni za kijeshi, kwa lengo kutanua wigo wa utawala wake.

Kulingana na simulizi za Kihausa, Malkia Amina alikuwa ‘mwanamke aliyeishi kabla ya wakati wake.’

Katika filamu ya Netflix iitwayo Amina, iliyotolewa mwkaa 2021, mhusika mkuu anaonesha namna alivyoweza kupanda na kushika hatamu ya taji la Zazzau.

Hadi leo hii, bado haijulikani mahali alipofia wala kuzikwa malkia huyu.

Baadhi ya wanahistoria wanadai kuwa alifia nje ya eneo la Zazzau, pengine katika himaya ya Igala.

 

CHANZO:TRT Afrika
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us