AFRIKA
1 dk kusoma
Tanzania yamuachilia Agather, mwanaharakati wa Uganda
Agather Atuhaire alikamatwa pamoja na mwanaharakati wa Kenya Boniface Mwangi walipokuwa wameenda nchini humo kushuhudia kesi ya mwanasiasa wa upinzani Tanzania, Tundu lissu.
Tanzania yamuachilia Agather, mwanaharakati wa Uganda
Mwanaharakati wa Uganda Agather Atuhaire./Picha:Wengine / Others
23 Mei 2025

Mwandishi wa habari wa Uganda na mwanaharakati wa haki za binadamu Agather Atuhaire amepatikana akiwa hai baada ya siku kadhaa za kuzuiliwa nchini Tanzania bila mawasiliano.

Vyanzo vya habari nchini Uganda vinathibitisha kwamba alipatikana katika mpaka wa Uganda na Tanzania huko Mutukula Alhamisi usiku, akiwa katika hali mbaya na bila kuwepo na taarifa rasmi ya kuachiliwa kwake.

Atuhaire, ambaye alikamatwa Mei 19 jijini Dar es Salaam, hivi sasa yuko chini ya uangalizi wa marafiki na jamaa wanaomsaidia kurejea Kampala.

Kuachliwa kwake kunafuatia jitihada za ubalozi wa Uganda nchini Tanzanai kuiandikia serikali ya Tanzania rasmi huku ikiomba Agather aweze kutembelewa na maafisa wa ubalozi.

Agather amaeachiliwa baada ya mwanaharakati wa Kenya Boniface Mwangi pia kuachiliwa.


Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us