AFRIKA
1 dk kusoma
Karibu wachimba migodi 300 wakwama Afrika Kusini
Msemaji anasema wafanyakazi wote wako salama na wanajulikana waliko na kwamba wako katika mchakato wa kuwafikishia chakula.
Karibu wachimba migodi 300 wakwama Afrika Kusini
Msemaji wa kampuni anasema wafanyakazi wote wako salama na wanajulikana waliko. / Getty Images
23 Mei 2025

Kampuni ya uchimbaji madini ya Afrika Kusini ya Sibanye Stillwater imesema siku ya Ijumaa kuwa juhudi zinaendelea kuwaokoa wachimba migodi 289 waliokwama kwenye mgodi wake wa Kloof karibu na jiji la Johannesburg.

"Tunathibitisha kuwa kulikuwa na tukio katika mgodi wa Kloof 7 na tayari tunachukua hatua za kuhakikisha usalama wa eneo hilo ili tuweze kuwaleta wafanyakazi juu kutoka chini ya mgodi huo," alisema msemaji wa kampuni ya Sibanye.

Msemaji amesema kuwa wafanyakazi wote wako salama na wanajulikana waliko na kwamba kampuni hiyo iko kwenye mchakato wa kuwafikishia chakula.

"Tunatarajia tatizo hili litatuliwe leo," msemaji alisema.

Chama cha wafanyakazi wa migodini (NUM) mapema kilisema kuwa kimepata taarifa kuhusu tukio hilo, ambalo walisema lilitokea saa nne asubuhi za nchini humo siku ya Alhamisi.

CHANZO:TRT Afrika and agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us