AFRIKA
1 dk kusoma
Prof Janabi ashinda uteuzi wa Mkurugenzi wa WHO - Kanda ya Afrika
Prof Janabi, daktari wa magonjwa ya moyo na msimamizi wa afya anayeheshimika sana, amekuwa na jukumu muhimu katika kuunda hali ya matibabu ya Tanzania.
Prof Janabi ashinda uteuzi wa Mkurugenzi wa WHO - Kanda ya Afrika
Prof Mohammed Janabi anaipa Tanzania Ushindi wa pili wa nafasi hiyo baada ya Faustin Ndugulile aliyefariki kabla ya kuingia ofisini / others
18 Mei 2025

Profesa Mohammed Janabi ndiye Mkurugenzi mpya wa Shirika la Afrya Duniani WHO, kanda ya Afrika.

Prof Janabi amewashinda wagombea wengine wanne kutoka sehemu mbali mbali za Afrika kuchukua nafasi hiyo iliyoachwa wazi kufatia kifo cha Daktari Faustine Ndugulile, muda mfupi kabla ya kuingia ofisini.

Wizara ya Afya Tanzania imetuma pongezi kwa Profesa Janabi n akumsifia kama mgombea aliyestahiki.

‘‘Tunafurahia kuchaguliwa kwa Prof. Mohamed Janabi kuwa Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika’’ ! Shukrani kwa Afrika kwa uungwaji mkono wa kiwango cha juu,’’ iliandika wizara hiyo.

Prof Janabi, daktari wa magonjwa ya moyo na msimamizi wa afya anayeheshimika sana, amekuwa na jukumu muhimu katika kuunda hali ya matibabu ya Tanzania. Uzoefu wake ni wa miongo kadhaa, ikiwa ni pamoja na kuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na baadaye Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Profesa Momammed Janabi amewapiku wagombea wengine, N’da Konan Michel - Ivory Coast, Mohammed Lamine - Guinea, Dkt Boureima Hama Sambo - Niger, Professor Moustafa Mijiyawa wa Togo.

CHANZO:TRT Afrika Swahili
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us