AFRIKA
1 dk kusoma
Gabon yamhamishia kifungo cha nyumbani mke na mtoto wa Rais wa zamani Bongo
Kuhamishiwa kifungo cha nyumbani - ambapo sasa wameunganishwa tena na Ali Bongo - kulikuja Mei 9 baada ya shinikizo kutoka kwa maafisa wa Umoja wa Afrika kuwaachilia.
Gabon yamhamishia kifungo cha nyumbani mke na mtoto wa Rais wa zamani Bongo
familia ya rais wa zamani wa Gabon Ali bongo / TRT Afrika / TRT Afrika Français
15 Mei 2025

Mke na mtoto wa rais wa zamani wa Gabon wamehamishwa kutoka jela hadi kifungo cha nyumbani, ingawa haijulikani ni lini wanaweza kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za uhalifu wa kifedha, vyanzo viwili viliiambia Reuters.

Sylvia Bongo, 62, na Nourredin Bongo, 33, walitiwa mbaroni muda mfupi baada ya Ali Bongo kupinduliwa katika mapinduzi ya kijeshi zaidi ya mwaka mmoja na nusu uliopita.

Hivi majuzi walikuwa wamezuiliwa katika vyumba vya chini ya ardhi katika ikulu ya rais huko Libreville, moja ya vyanzo vilisema.

Kuhamishwa kwa kifungo cha nyumbani - ambapo sasa wameunganishwa tena na Ali Bongo - kulikuja Mei 9 baada ya shinikizo kutoka kwa maafisa wa Umoja wa Afrika kuwaachilia.

Mnamo Mei 1, moja ya vyanzo vilisema, walikuwa wamelazwa hospitalini baada ya kufanya mgomo wa kula.

Sylvia Bongo na Nourredin Bongo wanatuhumiwa kwa uhalifu ikiwa ni pamoja na utakatishaji fedha.

Wanaowaunga mkono wamesema waliteswa wakiwa kizuizini.

CHANZO:TRT Afrika and agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us