AFRIKA
1 dk kusoma
Ufaransa ‘yatupilia mbali’ kesi ya aliyekuwa mke wa Juvenal Habyarimana
Kulingana na mahakimu waliokuwa wanafuatilia kesi hiyo, hapakuwa na ushahidi wa moja kwa moja wa kumuhusisha na tukio hilo.
Ufaransa ‘yatupilia mbali’ kesi ya aliyekuwa mke wa Juvenal Habyarimana
Mke wa Juvenal Habyarimana
19 Mei 2025

Agathe Habyarimana alikuwa akihusishwa na kifo cha kiongozi huyo wa zamani wa Rwanda, kilichotokea Aprili 6, 1994.

Mwanamama huyo, ambaye amekuwa akiishi nchini Ufaransa toka mwaka 1998, aliikimbia Rwanda, siku chache baada ya kutunguliwa kwa ndege iliyokuwa imembeba mumewe, tukio lilopelekea kutokea kwa mauaji ya kimbari ambayo yalisababisha vifo vya watu 800,000 nchini humo.

Uchunguzi kuhusiana na chanzo cha kifo cha Habyarimana ulianza toka mwaka 2008 baada ya taasisi moja ya Ufaransa kufungua mashitaka dhidi ya Agathe, ambaye pia alihojiwa baada ya kushukiwa kuwa sehemu ya jamii wa Wahutu ambao waliendesha mauaji dhidi ya Watutsi.

Kulingana na mahakimu waliokuwa wanafuatilia kesi hiyo, hapakuwa na ushahidi wa moja kwa moja wa kumuhusisha na tukio hilo.

"Ingawa taarifa bado zinaendelea kuzagaa, haziwezi kuwa na ushahidi wa kutosha," walisema mahakimu hao.

CHANZO:TRT Afrika and agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us