AFRIKA
1 dk kusoma
Tume ya Uchaguzi Tanzania yasema hakuna muda wa ziada uandikishaji Daftari la Kudumu
Zoezi hilo pia linahusisha kuwaondoa wasio na sifa kwenye Daftari hilo.
Tume ya Uchaguzi Tanzania yasema hakuna muda wa ziada uandikishaji Daftari la Kudumu
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza na wakazi wa Kata ya Ubiri Wilayani Lushoto ambao walijitokeza kuhakiki taarifa zao katika Daftari la awali la Wapiga Kura lililobandikwa katika kituo cha Ofisi ya Kata hiyo leo Mei 20,2025. Jaji Mwambegele yupo Mkoani Tanga kuangalia mwenendo wa zoezi la ubpreshaji awamu ya pili. / TRT Afrika Swahili
20 Mei 2025

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi nchini Tanzania imewataka wananchi wenye sifa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha au kuboresha taarifa zao katika  Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya pili mzunguko wa pili ulioanza Mei 16 hadi 22, 2025.

Tume imesema kuwa haitaongeza muda baada ya zoezi hilo kukamilika ambalo pia linahusisha kuwaondoa wasio na sifa kwenye Daftari hilo.

Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele, ambae ni Mwenyekiti wa Tume, ameyasema hayo katika ziara ya kukagua mwenendo wa zoezi hilo katika Halmashauri za Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga.

Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us