AFRIKA
1 dk kusoma
Bunge la Uganda laidhinisha pendekezo la bajeti ya Dola Bilioni 20
Serikali imesema itaweka kipaumbele katika sekta ya kilimo-viwanda, utalii na madini.
Bunge la Uganda laidhinisha pendekezo la bajeti ya Dola Bilioni 20
Waziri wa Fedha Matia Kasaija anatazamiwa kuwasilisha bajeti hiyo bungeni rasmi Juni 12./Reuters
16 Mei 2025

Wabunge wa Uganda wameidhinisha bajeti iliyopendekezwa na serikali kwa mwaka wa fedha unaoanza Julai, huku matumizi yaliyopangwa yakiwa ya wastani ikilinganishwa na mwaka uliopita.

Kupitia mapendekezo hayo, Uganda itatumia Dola Bilioni 20 katika mwaka fedha wa 2025/26, ikiwa ni mabadiliko kidogo, kutoka kwa matumizi ya mwaka unaoishia mwezi ujao, ambayo ni shilingi trilioni 72.1, lilisema bunge la nchi hiyo katika taarifa yake iiyowekwa kwenye mtandao wa kijamii wa X mwishoni mwa Alhamisi.

"Bunge limezingatia na kupitisha mapendekezo ya bajeti ya mwaka ya fedha 2025/2026," ilisema taarifa hiyo.

Kulingana na serikali ya nchi hiyo, vipaumbele vya matumizi kwa mwaka ujao vitakuwa kwenye sekta ya kilimo, utalii na madini, ikiwemo mafuta ya petroli.

Waziri wa Fedha Matia Kasaija anatazamiwa kuwasilisha bajeti hiyo bungeni rasmi Juni 12 na kutoa maelezo zaidi kuhusu mahali pesa hizo zitatumika.

Uganda inatekeleza miradi ya miundombinu ili kuanza uzalishaji wa kibiashara wa mafuta ghafi mwaka ujao.

Miundombinu hiyo inajumuisha bomba la mafuta ghafi lenye thamani ya dola bilioni 5, kusaidia nchi hiyo isiyo na bandari kusafirisha mafuta yake kwenye masoko ya kimataifa kupitia Tanzania.


CHANZO:TRT Afrika and agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us