AFRIKA
1 dk kusoma
Rais Ruto akabidhi nyumba za bei nafuu Kenya
Rais wa Kenya William Ruto siku ya Jumatano alikabidhi familia 1080 nyumba za bei nafuu katika mtaa wa Mukuru, mji mkuu wa Kenya, Nairobi.
Rais Ruto akabidhi nyumba za bei nafuu Kenya
Rais Ruto anasema mradi huo wa mtaa wa Mukuru utakuwa na jumla ya nyumba 13, 248 utakapokamilika. / Others
20 Mei 2025

Moja ya ahadi za rais William Ruto wa Kenya wakati wa kampeni zake za 2022 ilikuwa ni ujenzi wa nyumba za bei nafuu kwa wananachi wa Kenya, ikiwa lengo ni kuinua watu wa kipato cha chini.

Katika halfa ya makabidhiano Jumatano rais Ruto alieleza furaha yake kwa kutimiza ahadi ambayo ni sehemu ya mpango wa ujenzi wa nyumba 200,000 kila mwaka, kulingana na mradi huo. “Hii ni siku muhimu sana kwangu tangu nilivyoanza kufanya siasa!”, alisema Ruto.

Rais Ruto anasema mradi huo wa mtaa wa Mukuru utakuwa na jumla ya nyumba 13, 248 utakapokamilika.

Katika ilani ya chama chake ya miaka 5, Ruto analenga kujenga jumla ya nyumba milioni moja zitakazokuwa makazi ya watu zaidi ya milioni tano.

Wakati wa kuwakabidhi funguo za nyumba Ruto alisema mradi huo ambao wamekuwa wakiupinga sasa ni dhahiri kuwa unaleta mafanikio.

Raia wengi wamekuwa wakiutaja mradi huo kuwa tata kutokana na kodi ya lazima iliyoanzishwa na serikali katika kufadhili mradi wa nyumba za bei nafuu, wakilalamika kuwa ufisadi utakithiri katika mipango kama hiyo, huku rais akitetea serikali yake kuwa na nia njema ya kuwaondoa watu kutoka mitaa ya mabanda na kuwapa makazi yenye hadhi.

CHANZO:TRT Afrika
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us