Barani Afrika, kuna eneo linalosifika kuwa na joto zaidi ulimwnguni.
Likiwa linapatikana kaskazini mwa Ethiopia, eneo hilo si jingine bali ni Bonde la Danakil.
Eneo hili linapatikana katika jangwa la Danakil, kando ya mipaka ya Eritrea na Djibouti.
Hali ya joto katika eneo hilo inakadiriwa kufikia nyuzi joto 35, wakati mwingine hufikia 50.
Kwa mwaka, eneo hili hupata wastani wa mvua ya kati ya milimita 100 na 200.
Eneo la Danakil pia linatambulika kuwa sehemu hatari zaidi duniani, yumkini ndio fahari yake. Bonde hilo ni moja ya maeneo ya chhini kabisa duniani, likiwa takribani mita 100 chini ya usawa wa bahari.
Ardhi ya eneo hili ni nyembamba, ikiwa ni matokeo ya mlipuko wa volkano.
Danakil ni kivutio kikubwa cha utalii nchini Ethiopia, hasa kwa wale wanaoweza kustahimili kiwango cha juu cha joto.
Hapa kuna mazingira ya ajabu kama maziwa yenye chumvichumvi, mbayo hukaa kwenye sehemu za volkeno.
Mchanganyiko wa rangi za manjano, machungwa, nyekundu, bluu na kijani hutokana na mvua na maji ya bahari kutoka ukanda wa pwani ya karibu ambayo hupenya hadi kwenye maziwa ya sulfuriki na kupata joto.
Joto linapofukiza maji, amana za rangi zinazofanana na ukoko hukua katika nchi nzima, na kuchanganyika katika maziwa baridi.
Maziwa haya yanaitwa "maziwa ya kuuwa."Hapa pia kuna Volkano hai inayoitwa Erta Ale
ikimaanisha "Mlima wa Kuvuta Moshi" kwa lugha ya ndani ya Afar.
Hili ni kati ya maziwa nane yenye kutoa uji uji wa lava ulimwenguni.
Ni jambo la kawaida kuona wadudu na ndege waliokufa pembezoni mwa chemchem za salfa za Danakil, jambo ambalo
linahusishwa na wao kunywa maji hayo au kuvuta hewa nyingi ya kaboni dioksidi.
Kutokana na hali yake ya joto, inashauriwa kutembelea eneo hili kati ya miezi Novemba na Machi, wakati hali ya joto inaposhuka hadi kufikia wastani wa nyuzi joto 25.
Watu wanaoishi katika maeneo haya wanaitwa Afar, ambao wana utamaduni wa kuhama hama, huku shughuli yao ya kiuchumi ikiwa ni uchimbaji madini, usafirishaji na uuzaji wa chumvi.