AFRIKA
2 dk kusoma
Mali ya mamia ya milioni yateketea katika moto mkubwa wa soko la nguo kuu kuu la Gikomba, Kenya
Mpangilio duni na msongamano wa vibanda na maduka zimesababisha visa vingi vya moto katika soko hili kubwa zaidi nchini Kenya na hasara ya mamia ya milioni ya pesa.
Mali ya mamia ya milioni yateketea katika moto mkubwa wa soko la nguo kuu kuu la Gikomba, Kenya
Wafanyabiashara waliopoteza hisa zao katika moto huo walishuku kuwa nyaya za umeme zenye hitilafu zinaweza kuwa sababu. / TRT Afrika Swahili
18 Mei 2025

Wafanyibiashara wa nguo, viatu na mali zingine kuu kuu katika soka la Gikomba, jijini Nairobi wanahesabu hasara yao kwa mara nyingine baada ya moto wa asubuhi kuteketeza vibanda vyao na kuharibu mali ya mamilioni ya pesa.

Japo sababu ya moto huo bado haijabainishwa, maelezo ya awali ni kuwa moto huo ulianza mwendo wa saa tisa usiku na kusambaa haraka kupitia sehemu ya viatu iliyo karibu na barabara ya Lamu eneo la Pumwani, Majengo.

Mbunge wa ene hilo Yusuf Hassan alithibitisha kisa hicho, na kusema kuwa wazima moto wa kaunti na watu wa kujitolea wa eneo hilo walijibu haraka kukabiliana na moto huo.

"Tunashukuru hatua za haraka zinazochukuliwa na huduma za dharura, lakini ni lazima tushughulikie sababu kuu za moto huu unaotokea mara kwa mara," alisema.

Hakuna majeruhi

Polisi walisema hakuna majeruhi au majeraha yaliyosababishwa moja kwa moja na tukio hilo.

Mpangilio duni na msongamano wa vibanda na maduka zimesababisha visa vingi vya moto katika soko hili kubwa zaidi nchini Kenya na hasara ya mamia ya milioni ya pesa.

Kisa cha hivi punde zaidi kilitokea Aprili 1 wakati moto mwingine ulizuka takriban saa 3:00 asubuhi katika sehemu ya Kwa Mbao sokoni.

Moto huo uliteketeza eneo lote na kusambaa hadi kwenye kituo cha mabasi jirani.

CHANZO:TRT Afrika and agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us