Shughuli mbalimbali zimefanyika kama sehemu ya Maadhimisho ya Mei 19 ya Siku ya Ataturk, Vijana na Michezo, ikiwa ni miaka 106 ya Mustafa Keman Ataturk ya kuwasili Samsun Mei 19, 1919, kuanzisha vita vya uhuru.
Jumapili asubuhi, watu kutoka sehemu mbalimbali ya nchi walikusanyika kutoa heshima kwa kiongozi mkuu huku Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan akigusia umuhimu wa kuwawezesha vijana katika siku hiyo ya historia.
Erdogan amesema Uturuki itatoa fursa kwa vijana kutambua uwezo wao katika kila nyanja-kuanzia sayansi na Sanaa, michezo na kilimo, diplomasia na teknolojia ya nuklia-na itaendelea kwenda nao sambamba.
Katika mji mkuu wa Ankara, maelfu walitembelea kaburi la Mustafa Kemal Ataturk.
Maadhimisho yalianza kwa kukaa kimya na wimbo wa taifa, na kufuatiwa na ujume ulioongozwa na Waziri wa Vijana na Michezo Osman Askin Bak, akiungana na mwakilishi wa vijana kutoka sehmu mbalimbali za nchi.
“Umewasha taa ya uhuru Samsun miaka 106 iliyopita; leo, taa hiyo hiyo emeenea kote katika hii ardhi kama ishara ya umoja, utulivu na matumaini,” Bak aliandika.
Kujenga mustakbali wa nchi
Mei 16, 1919, Ataturk aliondoka Istanbul akiwa amepanda feri ya Bandirma.
Siku tatu baadae, Mei 19, aliwasili katika gati ya Dil (Reji) mjini Samsun-tarehe ambayo leo inaangaliwa na wote kama mwanzo wa Vita vya Uhuru wa Uturuki.
Wakati huo, alikuwa ameteuliwa na serikali ya Ottoman kama Inspekta Jenerali wa jeshi la Ottoman, ambalo lilikuwa na shinikizo kutoka kwa vikosi vya washirika kutoka Istanbul.
Badala ya kufuata maagizo rasmi, Ataturk alianzisha vuguvugu ya taifa ya kuwaondoa wageni na kujenga upya musktabali wa Anatolia.
Hii ilisababisha vita vya miaka minne ambavyo mwishoni viliisha kwa kuanzishwa kwa Jamhuri ya Uturuki 1923.
Mwaka 1938, Ataturk aliifanya Mei 19 kama Siku ya Vijana na Michezo, alionyesha umuhimu wa jukumu la vijana katika kujenga mustakbali wa nchi.
Katika mji wa Samsun, meli ya jeshi ya Uturuki TCG Anadolu iliwasili ikiwa imebeba vijana 81 wanaowakilisha kila mkoa na chuo cha mafunzo ya jeshi.