Makadinali na wafuasi wanahudhuria Misa Takatifu, kuadhimisha kuchaguliwa kwa papa mpya katika Kanisa la St. Peter, Basilica, Vatican, Mei 7, 2025.
Itakapofika saa kumi na moja jioni EAT, makadinali 133 watakaopiga kura watakusanyika katika Kanisa la Pauline Chapel na kufanya msafara hadi Sistine Chapel huku wakiimba.Wakifika Kanisa la Sistine, makadinali watakula kiapo cha usiri.
Baada ya hapo Mkuu wa Maadhimisho ya Kiliturujia ya Kipapa Diego Ravelli atatangaza “extra omnes” (“kila asiyepaswa kuwa hapa atoke nje”).Tamko hilo la “extra omnes” huashiria mwanzo wa mkutano.