Kwa nini uchaguzi wa papa hugubikwa na usiri?
Kwa nini uchaguzi wa papa hugubikwa na usiri?
Makadinali hufungiwa ndani ya kanisa na kunyang’anywa vifaa vyao vya mawasiliano ili kuwaepusha kufanya mawasiliano na ulimwengu wa nje ikiwemo waandishi wa habari.
6 Mei 2025

Mei 7 mwaka huu, kongamano la Makardinali, yaani Conclave litakutana ndani ya kanisa la Sistine, lilipo ndani ya Vatican, kwa ajili ya kuanza mchakato wa kumchagua Papa mpya.

Mchakato huo, unatarajiwa kuwa wa siri kubwa ndani ya milango ya kanisa la Sistine, ambapo Makadinali hao hawatoruhusiwa kuingia na nyenzo zozote za mawasiliano kama vile simu au hata barua pepe, wakati wa kongamano hilo, huku milango ya kanisa hilo ikipigwa kufuli.

Desturi hii ilianza wakati wa vuguvugu la mwamko mpya barani Ulaya.

Makadinali hawa walifungiwa ndani ya kanisa la Sistine na kunyang’anywa vifaa vyao vya mawasiliano ili waepuke ushawishi wa viongozi wa dola ya Kirumi kwa kipindi hicho na familia zilizokuwa na nguvu na uwezo wa kifedha kwa kipindi hicho.

Hata hivyo, siku hizi, Makadinali hao hufungiwa ndani na kunyang’anywa vifaa vyao vya mawasiliano ili kuwaepusha kufanya mawasiliano na waandishi wa habari.

Kabla ya kukutana ndani ya kanisa la Sistine, Makadinali hao watafanya ibada maalumu, na kwa sasa wapo katika Novena ndani ya Basilica ya Mtakatifu Petro, tayari kabisa kwa uchaguzi huo unaosubiriwa na watu wengi ulimwenguni.

Baada ya hapo, Makadinali hao wanakula kiapo kikuu cha usiri, yaani hawatoruhusiwa kusema chochote kwa mtu yeyote yule kuhusu yale yanayofanyika wakati wa mchakato mzima wa kumchagua Papa mpya ndani ya kanisa la Sistine.

Muda wote, makadinali hawa watakuwa wanasindikizwa na makachero maalumu wengine wakiwa wamevalia mavazi ya Kiaskofu, na wengine mavazi ya kawaida, ili kuweza kubaini mienendo ya Makadinali hao wakati wa uchaguzi.

Ndani ya kanisa la Sistine, ibada mbalimbali zinafanyika, na Makadinali hao hupokezana zamu za kuongoza ibada hizo, kila baada ya siku tatu, inategemea na siku watakazo kaa ndani ya kanisa hilo, huku Makadinali hao wakipata huduma zote muhimu za kibinadamu kama vile vyakula, vinywaji na matibabu.

Ikumbukwe kuwa, conclave iliyokaa kwa muda mrefu zaidi ilikuwa kwenye karne ya 13, wakati kiti cha Papa kilipokaa wazi wa miaka 3, hadi Papa Gregory wa 10 alipochaguliwa mwaka 1271.

Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us