AFRIKA
1 dk kusoma
Jeshi la Sudan lasema RSF imelenga miundombinu karibu na uwanja wa ndege Port Sudan
Msemaji wa jeshi la Sudan amesema vikosi vya RSF vimelenga kambi ya jeshi la anga na miundombinu mengine karibu na eneo la uwanja wa ndege uliopo Port Sudan
Jeshi la Sudan lasema RSF imelenga miundombinu karibu na uwanja wa ndege Port Sudan
Mwanamke aliyekosa makazi nchini Sudan na watoto wake, baada ya mashambulizi ya RSF katika eneo la Zamzam, akiwa kambini katika mji wa Tawila, Kaskazini mwa Darfur, Aprili 15, 2025. / Reuters
4 Mei 2025

Msemaji wa Jeshi la Sudan amesema vikosi vya wapiganaji vya RSF vimelenga kwa mashambulizi kambi ya jeshi la anga pamoja na miundombinu mengine iliyopo karibu na eneo la uwanja wa ndege wa Port Sudan.

Haya yanajiri wakati Tume ya Kitaifa ya Kutetea Haki za Binadamu ya Sudan siku imetangaza kuuawa kwa raia wasiopungua 300, ikiwemo watoto 21 na wanawake 15, katika mashambulizi yaliyofanywa na kundi la RSF katika mji wa Al-Nahud kwenye jimbo la Kordofan Magharibi.

TRT Global - Idadi ya waliouawa katika shambulizi la Al-Nahud Sudan yafika 300: Tume ya haki

Tume ya kitaifa ya haki za binadamu nchini Sudan imeshtumu ‘ukiukwaji mkubwa uliotekelezwa na vikosi vya RSF dhidi ya raia huko Al-Nahud’

🔗

Katika taarifa rasmi, tume hiyo imelaani tukio hilo na kusema ni “ukiukwaji mkubwa uliotekelezwa na kundi la RSF dhidi ya raia wa Al-Nahud, ikiwemo kuwalenga kwa makusudi, kuwapiga risasi kwa karibu, na kuwaua.”

Tume pia ilisema kuwa idadi hiyo ya vifo ni ya muda tu kwa sasa kwa sababu bado mashambulizi yanaendelea katika mji huo kwa sababu wapiganaji wa RSF wanazuia misaada kuingia na kutoruhusu watu kuondoka eneo hilo.

Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us