Makadinali wa Kanisa Katoliki wameanza mchakato wa kumchagua papa mpya, ambapo watajitenga na ulimwengu hadi watakapomchagua kiongozi mpya wanaeamini anaweza kuunganisha Kanisa la kimataifa lakini lililogawanyika.
Makadinali hao wapo katika Kanisa la Vatican la Sistine Chapel na baada ya Misa ya hadhara katika Basilica ya Mtakatifu Petro wameanza mkutano wao wa usiri wa mrithi wa Papa Francis, aliyefariki mwezi uliopita.
Hakuna papa ambaye amechaguliwa katika siku ya kwanza ya kongamano kwa karne nyingi, kwa hivyo upigaji kura unaweza kuendelea kwa siku kadhaa kabla ya mmoja wa wakuu wa Kanisa wenye kofia nyekundu kupokea theluthi-mbili ya kura inayohitajika kumchagua papa wa 267.
Kutakuwa na kura moja tu siku ya Jumatano. Baada ya hapo, makadinali wanaweza kupiga kura mara nne kwa siku.
Watachoma kura zao, na moshi mweusi utatoka kwenye bomba la moshi kwenye paa ya Kanisa hilo ukiashiria kura ambayo haijakamilika, huku moshi mweupe na kengele zikiashiria kwamba waumini bilioni 1.4 wa kanisa hilo wamepata kiongozi mpya.
Ushawishi wa papa unafikia zaidi ya Kanisa Katoliki, ukitoa sauti ya maadili na wito kwa dhamiri ambayo hakuna kiongozi mwingine wa kimataifa anayeweza kulingana.
Katika Ibada ya Misa Takatifu iliyofanyika katika Kanisa kuu la Mtakatifu Petro Jumatano asubuhi kabla ya kuingia kwenye jumba hilo la ibada, makadinali hao walisali ili Mungu awasaidie kupata papa ambaye atafanya “uangalifu” duniani kote.
Katika mahubiri yake, Kadinali wa Kiitaliano Giovanni Battista Re aliwaambia wenzi wake kwamba lazima waweke kando "kila jambo la kibinafsi" katika kuchagua papa mpya na kukumbuka"... mema tu ya Kanisa na ya ubinadamu".
Re, Mkuu wa Chuo cha Makardinali, ana umri wa miaka 91 na hataingia kwenye mkutano huo, ambao umetengwa kwa ajili ya makadinali walio chini ya umri wa miaka 80.
Makadinali katika siku za hivi karibuni wametoa tathmini tofauti ya kile wanachotafuta kwa papa ajaye.
Wakati wengine wametaka kuendelea na maono ya Francis ya uwazi zaidi na mageuzi, wengine wamesema wanataka kugeuza saa nyuma na kukumbatia mila za zamani. Wengi wameonyesha kuwa wanataka upapa unaotabirika zaidi, uliopimwa.
Rekodi ya makadinali 133 kutoka nchi 70 wataingia katika kanisa la Sistine Chapel, kutoka 115 kutoka mataifa 48 katika kongamano la mwisho la mwaka 2013 -- ukuaji unaoakisi.