26 Machi 2025
Afisa kutoka ujumbe wa kimataifa wa usaidizi wa usalama wa Kenya (MSS) alitoweka nchini Haiti siku ya Jumanne baada ya tukio lililohusisha magenge, MSS ilisema katika taarifa.
Vikosi hivyo maalum vilishambuliwa na magenge vilipokuwa vikisaidia gari kutoka kwa polisi wa Haiti ambalo lilikwama kwenye mtaro, unaoshukiwa kuchimbwa na magenge, taarifa hiyo iliongeza.
Vyombo vya habari vya eneo hilo viliripoti kwamba askari huyo aliuawa, na video zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zilionesha mwili wa afisa ukiwa ardhini na umelowa damu.
Kikosi cha takriban polisi 800 wa Kenya kinaongoza ujumbe huo unaojumuisha wanajeshi na polisi kutoka nchi kama vile Jamaica, Guatemala na El Salvador ambao wanafanya kazi pamoja na Polisi wa Haiti.