MICHEZO
2 dk kusoma
Uganda, Tanzania zaendelea kusaka nafasi ya Kombe la Dunia 2026
Mechi za kuwania kufuzu kwa Kombe la Dunia 2026 zinaendelea huku timu kadhaa zikiingia uwanjani kutafuta nafasi hiyo.
Uganda, Tanzania zaendelea kusaka nafasi ya Kombe la Dunia 2026
Timu ya Taifa ya Tanzania. Picha: Reuters / Reuters
25 Machi 2025

Uganda wako nyumbani kuikaribisha Guinea ikiwa ni mechi ya Kundi G. Guinea ina alama 7 ikiwa katika nafasi ya tatu ya msimamo wa kundi hilo, alama tano nyuma ya Algeria na Msumbiji ambao wote wana alama 12 tofauti ni magoli.

“Mbweha wa Jangwani’, Algeria wana magoli mengi zaidi.

‘The Cranes’ ina alama 6 baada ya kucheza mechi tano na iko katika nafasi ya tano kwenye kundi hilo, wakiwa tu juu ya Somalia yenye alama moja pekee.

Na kama timu zote mbili zitahitaji kuwa na matumaini ya kufuzu kwa kombe la Dunia, basi mechi lazima kila upande utafute alama 3 watakapovaana katika uwanja wa Namboole baadaye Jumanne mjini Kampala.

Mechi ya Morocco na Tanzania ya kundi E itachezwa katika uwanja wa Stade Municipal katika mji wa Oujda, ulioko kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Taifa stars ina alama 6 sawa na Niger. Morocco iko juu ya msimamo wa kundi hilo na alama 12. Kundi hilo lina timu tano pekee kutokana na kujiondowa kwa Eritrea kwenye mechi hizo.

Taifa stars inahitaji japo sare iweze kufufua matumaini yake ya kuelekea kwa mashindano hayo 2026. Iwapo Morocco watashinda, watakuwa na alama 15 na huenda ikawa vigumu kwa timu zingine kuwafikia.

Timu tisa zitakazoongoza kila kundi zinafuzu moja kwa moja kwa Kombe la Dunia.

Michuano ya Kombe la Dunia 2026, inaandaliwa kwa pamoja na Marekani, Canada na Mexico.

CHANZO:TRT Afrika Swahili
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us