UTURUKI
3 dk kusoma
Waziri wa Mambo ya Nje Fidan kufanya ziara Marekani kwa mazungumzo muhimu
Ushirikiano katika masuala ya ulinzi, mazungumzo kuhusu vikwazo kwa Iran,Urusi na Korea Kaskazini maarufu CAATSA na kuangalia upya kuhusu kurejesha Uturuki kwenye mradi wa ndege za F-35 yote yatakuwa kwenye agenda.
Waziri wa Mambo ya Nje Fidan kufanya ziara Marekani kwa mazungumzo muhimu
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Fidan amewahi kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio 14 Februari wakati wa kongamano la 61 la Usalama la Munich. / TRT World
24 Machi 2025

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan anaelekea Marekani Machi 25 kwa ziara rasmi ya siku mbili ambapo atafanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio na maafisa wengine, huu ukiwa mkutano wa kwanza wa mawaziri hao wawili katika kuimarisha uhusiano kati ya mataifa haya mawili ya NATO washirika tangu kuingia madarakani kwa Rais wa Marekani Donald Trump.

Majadiliano hayo yataangazia masuala ya kuimarisha uhusiano kati ya Uturuki na Marekani na maandalizi ya ziara za kitaifa katika siku zijazo. Masuala muhimu ya kikanda ikiwemo Ukraine, Palestina, na Syria yatajadiliwa wakati pande zote zikiangazia fursa za ushirikiano.

Fidan anatarajiwa kusisitiza msimamo thabiti wa Uturuki kwa utulivu wa Syria na kuheshimiwa kwa uhuru wao kama nchi huku wakitoa wito wa kuondolewa kwa vikwazo dhidi ya Syria na kuimarisha ushirikiano katika juhudi za kutoa misaada na ujenzi upya wa wa nchi hiyo.

Utaratibu mzuri wa kukabiliana na Daesh na kuhakikisha usimamizi mzuri wa vituo vya kuzuia watu pale magaidi wa Daesh walipozuiliwa nchini Syria pia utajadiliwa.

Ushirikiano katika kukabiliana na ugaidi, hasa kuhusu magaidi wa PKK/YPG wanaoendesha shughuli zao chini ya "SDF" Kundi la Kigaidi la Fetullah (FETO), pia ni masuala yatakayojadiliwa kwenye mazungumzo hayo.

Mwanadiplomasia huyo mkuu wa Uturuki anatarajiwa kujadili juhudi za kidiplomasia za Uturuki katika kumaliza vita vya Urusi na Ukraine na utayari wake katika kuchangia kwenye mpango wa kumaliza vita unaoongozwa na Marekani.

Kuhusu suala la Palestina, Fidan anatarajiwa kusisitiza haja ya kuongeza juhudi za kuwepo kwa kusitishwa kikamilifu mapigano Gaza na kuweka mazingira ya kufikishwa kwa misaada, akitaka Marekani kutumia ushawishi wao kwa Israeli.

Uhusiano wa mataifa mawili

Ushirikiano katika masuala ya ulinzi, itakuwa suala litakaloangaziwa zaidi, huku wakizungumza kuhusu vikwazo kwa Iran,Urusi na Korea Kaskazini maarufu CAATSA na kuangalia upya kuhusu kurejesha Uturuki kwenye mradi wa ndege za F-35.

Ujumbe wa Uturuki pia utajadili vizuizi kwa mchakato wa ununuzi katika sekta ya ulinzi huku maafisa wakiangazia uwezekano wa kuimarisha ushirikiano ambao utasaidia kufikisha lengo la biashara la dola bilioni $100.

Uhusiano wa mataifa haya mawili kati ya Uturuki na Marekani ulikuwa mzuri zaidi mwaka wote wa 2024, na unaendelea hivyo hivyo chini ya uongozi wa Trump.

Hivi karibuni Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alifanya mazungumzo kwa njia ya simu na Rais Trump 16 Machi.

Fidan amewahi kukutana na Rubio 14 Februari wakati wa kongamano la 61 la Munich kuhusu Usalama.

Mchakato wa manunuzi wa ndege za kivita za F-16 umepiga hatua, na tayari muda wa bunge la Congress kupata taarifa ulikamilika 11 Februari, 2024, na barua ya makubaliano kutiwa saini 3 Juni, 2024.

Makundi kadhaa ya ushirikiano yameanzishwa kuimarisha ushirikiano, ikiwemo lile la Syria (ambalo limekutana mara tatu, hivi karibuni ikiwa Januari 2025), mashauriano kuhusu nishati na tabianchi, kukabiliana na ugaidi, na kundi kuhusu Iraq, ikionesha namna gani ushirikiano kati ya mataifa haya mawili ya NATO washirika yalivyokuwa jumuishi.

CHANZO:TRT World
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us