AFRIKA
2 dk kusoma
Wakimbizi wa DRC nchini Burundi wafikia idadi kubwa
Idadi ya wakimbizi waliosajiliwa wanaohitaji msaada wa chakula imeongezeka maradufu na kufikia zaidi ya 120,000 kuanzia mwezi Januari 2025 huku vikosi vya serikali ya DRC vikipambana na kundi la waasi wa M23
Wakimbizi wa DRC nchini Burundi wafikia idadi kubwa
Wakimbizi kutoka DRC wanaendelea kuingia Burundi huku mashambulizi ya kikundi cha M23 katika maeneo ya Mashariki mwa DRC yakiendelea / AP
25 Machi 2025

Idadi ya wakimbizi wanaohitaji msaada wa chakula imeongezeka maradufu tangu mwezi Januari huku Shirika la Mpango wa Chakula Duniani likitahadharisha kuhusu ukosefu wa fedha.

Burundi inashuhudia idadi kubwa ya wakimbizi kwa miongo kadhaa ambapo maelfu wamekimbia maeneo ya mashariki mwa nchi jirani ya DRC, kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula, WFP.

Idadi ya wakimbizi waliosajiliwa wanaohitaji msaada wa chakula imeongezeka maradufu na kufikia zaidi ya 120,000 kuanzia mwezi Januari huku vikosi vya serikali ya Congo vikipambana na kundi la waasi wa M23 linalodaiwa kuungwa mkono na serikali ya Rwanda, tuhuma ambazo Rwanda imezikana.

M23 hivi sasa wanashikilia miji miwili mikubwa, WFP imesema katika taarifa yake.Wengi wa wakimbizi hao ni wanawake na watoto.

Mgogoro wa miongo kadhaa mashariki mwa Congo umeongezeka Januari, pindi M23 ilipochukua udhibiti wa mji wa kimkakati wa Goma, ukifuatiwa na mji wa Bukavu mwezi Februari.

Bukavu iko umbali usiozidi maili 30 kutoka mpaka wa Burundi.Marais wa Congo na jirani yake Rwanda walikutana wiki iliyopita nchini Qatari kwa mazungumzo yao ya kwanza ya moja kwa moja.

Mamilioni wakosa makazi
M23 ni moja ya takriban makundi 100 yenye silaha ambayo yanataka kushika himaya ya eneo lenye utajiri wa madini.

Mgogoro huo, umesababisha moja ya majanga mabaya ya kibinadamu duniani, huku kukiwa na zaidi ya watu milioni 7 waliokosa makazi.

WFP imeonya kwamba fedha zilizopo kwa uendeshaji wake nchini Burundi hazitoshi na kuna uwezekano zitaishi ifikapo mwezi June.

Imesema itaweza “kusitisha kabisa msaada wa chakula” kuanzia mwanzoni mwa Julai.

CHANZO:TRT Afrika and agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us