Mechi ya Sudan ilichezwa nchini Libya, ikiwa ndiyo kama yao ya nyumbani. Mechi zao zote zimechezwa viwanja vya nje kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe vinavyoendelea nchini kwao.
Jirani zao Sudan Kusini waliwaliza kwa kukomboa goli katika dakika 98 matokeo kuwa 1-1 na sasa wako katika nafasi ya tatu ya kundi B. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inaongoza kundi hilo baada ya kuwafunga Mauritania 2-0., wakiwa na alama 13. Senegal wako nafasi ya pili na alama 12 pia.
Ilikuwa usiku mbaya kwa Tanzania walipofungwa 2-0 na Morocco huko Oujda katika mechi ya kundi E. Morocco inaongoza kundi hilo ikiwa na alama 15. Niger na Tanzania wana alama 6 kila mmoja.
Uganda waliwapa cha kufurahia mashabiki wao wa nyumbani walipoifunga Guinea 1-0 mjini Kampala. Wako kwenye nafasi ya nne ya kundi G na alama 9 sawa na Botswana. Algeria wanaongoza kundi hilo na alama 15.
Katika kundi A Misri ina jumla ya alama 16 baada ya kuwafunga Sierra Leone 1-0 jijini Cairo. Burkina Faso ni ya pili na alama 11 huku Sierra Leone ikiwa nafasi ya tatu na alama 8.