2023 Kenya Airways ilipata hasara ya dola milioni 175 (shilingi bilioni 22.6) na kupata faida ni ishara kuwa shirika limeimarika katika kipindi cha miaka 12.
‘‘Mapato yetu kabla ya kodi ya riba yalikuwa asilimia 20 mwaka 2024 ikiwa ni zaidi ya wastani wa mashirika mengi katika sekta hii ambao ni asilimia 17, kuonesha ishara ya hali nzuri kwetu’’, alisema Afisa Mkuu Mtendaji Mkuu wa shirika hilo Allan Kilavuka
Idadi ya abiria kwa shirika hilo pia iliongezeka kwa asilimia 4 hadi kufikia milioni 5.23 mwaka huo. Usafirishaji wa mizigo pia uliongezeka kwa asilimia 25.
Kilavuka amesema faida hii itaelekezwa kwenye uwekezaji zaidi, akiongeza kuwa shirika hilo bado liko kwenye mikakati ya kupata wawekezaji zaidi ili liweze kuwa na uthabiti wa muda mrefu.
Serikali ya Kenya ina hisa nyingi zaidi kwenye shirika hilo asilimia 48.9, huku shirika la ndege la KLM likiwa na asilimia 7.8 na wadau wengine asilimia 2.8.