Angola itajiuzulu wadhifa wake kama mpatanishi kati ya pande zinazohusika katika mashambulizi ya waasi wanaodaiwa kuungwa mkono na Rwanda yanayoendelea mashariki mwa Jamhuri ya Kideomkrasia ya Congo,DRC.
Ilipewa jukumu hili na Umoja wa Afrika mwaka 2023.
Hii ni kwa mujibu wa ofisi ya rais wa nchi hiyo.
Waasi wa M23 walizidisha mzozo wao wa muda mrefu mwaka huu, na kuteka miji miwili mikubwa mashariki mwa DRC tangu Januari 2025 na kuvamia eneo lenye utajiri wa madini kama vile dhahabu na tantalum.
Akiwa Mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika (AU), Rais wa Angola Joao Lourenco amekuwa akijaribu kuipatanisha DRC na Rwanda ambazo zimekuwa na mzozo kuhusu mashambulizi hayo. DRC imekuwa ikiishutumu Rwanda kwa kuunga mkono kikundi cha M23.
Lakini Rwanda imekuwa ikikana tuhuma hizo.
"Angola inazingatia haja ya kujiondoa kutoka kwa jukumu la mpatanishi wa mzozo huu" "kujitolea zaidi" kwa vipaumbele vya jumla vya Umoja wa Afrika ,” ofisi ya rais wa Angola ilisema katika taarifa iliyotaja mkutano "uliositishwa" huko Luanda.
Urais huo uliangazia maendeleo yaliyopatikana Desemba 2024, wakati DRC ilikubali kutokomeza wanamgambo wa FDLR ambao ni adui ya rwanda na Rwanda iliahidi kuondoa vikosi vyake vya ulinzi kutoka DRC.
Ahadi hizi zilikusudiwa kuandaa mkutano wa kilele mnamo 15 Desemba 2025 huko Luanda - mkutano ambao hatimaye ulishindwa kufanyika kutokana na kutokuwepo kwa Rwanda.
“ Angola imejitolea kwa umakini, nguvu, na rasilimali, kwa lengo la kufikia amani ya kudumu mashariki mwa DRC na kurekebisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili jirani," ilisema taarifa hiyo.
Angola pia ilielezea kwamba ilikuwa imepanga mazungumzo ya moja kwa moja kati ya serikali ya DRC na waasi wa M23, na pande zote mbili ziliridhia duru ya kwanza ya mazungumzo iliyopangwa kufanyika Machi 18, 2025, mjini Luanda.
Hata hivyo, M23 ilikataa dakika ya mwisho ikishutumu vikwazo vya Umoja wa Ulaya dhidi ya M23 na maafisa wa Rwanda.
Baadaye Rais Paul Kagame wa Rwanda na Felix Tshisekedi wa DRC walionekana wakiwa wamekutana na Amir wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani, ambapo wawili hao waliunga mkono usitishaji wa vita mashariki mwa DRC.
Hata hivyo, ofisi ya Rais ilisema mchakato huo uliporomoka "dakika za mwisho" kutokana na "mchanganyiko wa mambo, miongoni mwao mambo ya nje na watendaji nje ya mchakato wa Afrika unaoendelea."
"Angola daima imekuwa ikiamini katika umuhimu wa mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Serikali ya DRC na M23," taarifa hiyo iliendelea.
"Tulifanya kazi ili kuwezesha hilo kwa idhini ya pande zote mbili ... lakini mchakato huo ulisitishwa kwa msimamo mkali."
Huku Angola ikijiweka kando, mustakabali wa juhudi za upatanishi bado haujulikani.
Umoja wa Afrika unatarajiwa kuteua mpatanishi mpya,