Serikali ya Namibia imewataka Wamarekani ambao wangependa kuitembelea nchi hiyo kuwa na Viza kabla ya kuingia nchini humo.
Mpango huo unatarajiwa kuanza kutekelezwa Aprili 1, 2025.
Katika tangazo lake, ubalozi wa Marekani nchini Namibia umewataka raia wake kuwa tayari kwa mabadiliko hayo na kuanza kufanya michakato ya kuomba kibali hicho cha kuishi nchini Nambia kwa njia ya mtandao.
Nchi nyingine ambazo raia wake wanapaswa kuwa na viza kabla ya kuingia Namibia ni pamoja na Canada, Ujerumani na Uingereza na zingine 29.
Mpango huo unalenga inalenga kuleta uwiano kati ya nchi za Afrika kwenye masuala ya usafiri.
“Namibia ilijaribu kuweka mazingira wezeshi kwa wageni wanaotutembelea. Hata hivyo, nchi hizo zimeshindwa kurudisha fadhila hiyo,” alisema Waziri wa Mambo ya Ndani, Uhamiaji, Ulinzi na Usalama, katika taarifa yake ya mwezi Mei 2024.
“Kutokana na utofauti huu, serikali italazimika kuweka mahitaji ya Viza ili kuleta usawa wa kidiplomasia.”