“Mijadala ya wiki iliyopita inaonesha kuwa usalama wa Ulaya bila uwepo wa Uturuki ni jambo lisilowezekana,”alisema Rais Erdogan baada ya mkutano wa Baraza la Mawaziri jijini Ankara siku ya Jumatatu.
"Mahitaji ya Ulaya kwa nchi yetu yanajidhihirisha, sio katika nyanja ya usalama tu, bali maeneo mengine pia kuanzia uchumi, diplomasia, biashara na maisha ya kijamii," aliongeza.
"Uturuki ipo tayari kuendeleza ushirikiano wake na nchi za Ulaya pamoja na Umoja wa Ulaya, katika mpango utakaofanikisha maslahi yanayofanana," amesema Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki,” aliongeza.
Uhusiano kati ya Marekani na Uturuki
Akiangazia uhusiano wa Ankara na Washington, Erdogan alisema kuwa inawezekana kwa uhusiano huo kupata mwelekeo tofauti wakati wa awamu ya pili ya Rais Donald Trump.
Kulingana na Erdogan, katika mazungumzo yake ya simu na Rais Trump, wawili hao walijadiliana mambo mengi muhimu ikiwemo kuondoa vikwazo vya kufikia malengo ya biashara ya Dola Bilioni 100.
Machi 16 mwaka huu, Erdogan na Trump walikuwa na mazungumzo kwa njia ya simu ambapo Rais wa Uturuki alionesha imani yake kuwa Ankara na Washington zitaimarisha mahusiano yao.