Utajiri wa Afrika: Mlangilangi, chanzo cha manukato
Utajiri wa Afrika: Mlangilangi, chanzo cha manukato
Maua ya mlangilangi maarufu kwa lugha ya Kiingereza ylang ylang ni asili ya mali ghafi muhimu kwa kutengeza manukato.
25 Machi 2025

Afrika ina mchango mkubwa katika uzalishaji wa manukato duniani.

Visiwa vya Comoro and Madagascar kwa mfano, katika bahari ya hindi vinaongoza kwa kuzalisha maua ambayo yanatumika kutengeneza manukato.  

Maua hayo ni ya mlangilangi maarufu kwa lugha ya Kiingereza ylang ylang ambayo ni mali ghafi muhimu ya kutengeza manukato.

Na ni kati ya vyanzo vikuu vya mapato kwa nchi hizo. 

Kwa mfano, mwaka 2022, Comoro ilivuna kiasi cha Dola za Kimarekani milioni 5.56 kutokana na mauzo ya maua hayo, hivyo kuifanya kuwa msafirishaji mkubwa wa 52 wa mafuta hayo ulimwenguni.

Katika mwaka huo huo, ilikuwa bidhaa ya 4 iliyouzwa nje nchini Comoro.

Miti wa mlangilangi hukua haraka, na kwa kawaida hufikia urefu wa wastani wa mita 12, ingawa baadhi ya miti inaweza kukua hadi mita 42.5. Ingawa wakulima hupunguza urefu wa mti ili iwe rahisi kwao kufikia maua.

Mlangilangi unachukua kati ya miaka 3-4 kuanza kuchanua. Mara ya kwanza, uvunaji unafanyika mara mbili kwa mwaka; kadri mti unavyokomaa, basi uvunaji wake utakuwa wa mara kwa mara. Maua ya mlangilangi hubadilika rangi yanapokua.

Huanza yakiwa na rangi ya manjano ya kijani kibichi na polepole hegeuka na kuwa manjano iliyoiva.

Maua ya mlangilangi hutoa harufu yake kali zaidi usiku. Ili kunasa harufu hiyo katika kilele chake, maua ya mlangilangi huchumwa jua linapochomoza tu na kisha kupelekwa kwa ajili ya usindikaji.

Katika kilele cha msimu wa kuchanua, wachumaji wanaweza kukusanya kilo 25 hadi 40 za maua kwa siku.

Maua mabichi yaliyovunwa husafirishwa hadi kwenye kiwanda cha usindikaji ambapo mara nyingi mafuta yanazalishwa kwenye vitengo vidogo vya ufundi vilivyochomwa moja kwa moja na kujitokeza kwa mvuke wa maji. Ukubwa wa chombo cha usindikaji hutofautiana kwa ukubwa wa kuanzia lita 150-500. 

Maua sharti yasindikwe ndani ya saa mbili baada ya kuvunwa. Kabla ya kuongeza maua, maji huwekwa kwenye chombo hadi kiwango cha kuchemka. Maua hupakiwa ili kuchukua takriban theluthi moja ya chombo. 

Usindikaji hufanywa kwa saa 18-24, kulingana na ukubwa wa chombo na uzoefu wa mtu binafsi. Inachukua takriban kilo 90 ya maua ya mlangilangi kutengeneza hadi lita mbili ya mafuta.

Mafuta zaidi yanaweza kupatikana usindikaji zaidi ukifanyika. Na hapa sasa mafuta muhimu ambayo hutumika kutengeneza manukato yanauziwa nchi kama Ufaransa, Marekani, Uswizi na Uingereza. 

Halafu unarudi tena barani Afrika baada ya kutumika katika utengezaji wa ile “designer perfume” ambayo inakufanya uonekana mtanashaki unapokuwa mbele za watu.

Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us