Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amezindua kitabu cha mkakati wa viwanda na teknolojia wa Uturuki wa mwaka 2030, wenye kulenga kuongeza hali ya nchi kujitegemea kiteknolojia na kiviwanda. Mkakati unaangazia masuala ya anga, ulinzi, kompyuta, nishati ya nyuklia na akili mnemba.
Akizungumzia mkakati huo, Erdogan alisisitiza kuwa mkakati huo unalenga kuiweka Uturuki katika ramani ya ubunifu, uzalishaji na viwanda vya kiteknolojia.
"Tumepiga hatua kubwa kwenye kujitegemea kiteknolojia," alisema Erdogan. "Sio tu itakuwa kiongozi wa kanda, lakini pia kinara katika teknolojia, ubunifu na uzalishaji wa viwandani."
Usalama na masuala ya anga: Ndege ya kivita ya Kaan
Uturuki inalenga kuzindua teknolojia ya anga ili kuiwezesha kuwa na anga yenye nguvu kiiteknolojia. Mkakati huu unaendana na matakwa ya nchi kwenye masuala ya anga, ikiwemo maendeleo ya satelaiti.
"Tutazindua mradi wa anga ili tuwe imara kwenye eneo hilo," alisema Erdogan. "Ndege yetu ya kivita ya Kaan itaimarisha sekta yetu ya ulinzi."
Hali kadhalika, Erdogan alitangazania ya kuunganisha mifumo ya ulinzi wa anga, chini ya mfumo unaojulikana kama ngao ya chuma, ili kuimarisha uwezo wa Uturuki wa kijeshi.
"Tukiwa na Celik Kubbe, tutakuwa na uwezo kunganisha mifumo yetu ya kiulinzi pamoja, ili kuongeza ufanisi wao," aliongeza.
Mikakati ya uwekezaji wa viwanda
Ili kuunga mkono uwekezaji huu, Uturuki itajenga maeneo maalumu ya majengo ya viwanda, kwa kutumia teknolojia za kisasa.
"Tutajenga maeneo maalumu ya majengo ya viwanda yenye miundombinu yenye uhakika ili kufanya viwanda vyetu viwe shindani," alisema Erdogan.
Huduma za Afya: Kukuza uzalishaji wa dawa
Kupitia program hii, Uturuki inalenga kuimarisha utafiti kwenye eneo la afya na kuongeza uzalishaji wa ndani wa dawa.
Manunuzi ya umma yatatumika ili kusaidia kampuni za dawa na hatimaye kupunguza uagizaji wa nje.
"Tutatumia mfumo wa manunuzi ya umma ili kuongeza uwezo wetu wa kitafiti," alisisitiza Erdogan.
Maandalizi ya teknolojia zijazo
Serikali inalenga kuanzisha taasisi yenye kukuza rasilimali watu nchini Uturuki, eneo ambalo litaleta mapinduzi kwenye uchakataji habari na usalama.
"Tunaanzisha taasisi hiyo ili kuongeza uwezo wa nchi yetu katika utafiti," alitangaza Rais Erdogan.
Hali kadhalika, uwekezaji kwenye kompyuta yenye kuendeshwa kwa Akili Mnemba itaongeza uwezo wa Uturuki, hasa katika eneo la sayansi ya data.
"Miundombinu yetu itakuwa ya viwango vya juu kwa kutumia hizo," alisema.
Nishati ya nyuklia
Rais Erdogan pia alitangaza uanzishwaji wa eneo maalumu la nishati ili kuchagiza utafiti katika nyuklia. Mradi huo unalenga kuifanya Uturuki ijitegemee kama chanzo cha nishati.
"Tutaanzisha eneo hilo ili tufanikiwe kwenye nishati ya nyuklia," alisema.
Utafiti Antarctica
Uturuki inalenga kujenga kituo cha utafiti huko baada ya tafiti tisa za mafanikio. Mradi huu utafanikisha kwenye jitihada za kumaliza mabadiliko ya tabia nchi, uhai wa bahari na mazingira.
"Tumefanya tafiti tisa kwa mafanikio huko Antarctica, huku tukilenga kituo cha kudumu katika eneo hilo," alisema Erdogan.
Uzalishaji wa vipandikizi nchini Uturuki
Erdogan alisisitiza umuhimu wa uzalishwaji wa vipandikizi hivyo, akisema kuwa Uturuki itaanza kutengeneza vitu hivyo nchini.
"Hili ni eneo muhimu sana, na tutahakikisha kuwa vyote vinafanyika nchini Uturuki," alisema.
Sekta ya magari: Kuimarisha uzalishaji wa ndani
Sekta hiyo itanufaika kupitia miradi ya ufadhili, ili kuhakikisha kuwa Uturuki inakuwa kitovu cha uzalishaji magari. Uturuki pia inalenga kuanza kutengeneza nishati safi miaka ijayo.
"Tunaimarisha sekta yetu ya kuzalisha magari kupitia miradi ya ufadhili," alisema Erdogan.
Kuhuisha vipaji
Kama sehemu ya mkakati wa muda mrefu, Uturuki itaanzisha mpango kabambe wa kuwataka wanasayansi wa Uturuki walio nje ya nchi kurudi nchini kwao.
"Mpango huo unalenga kuwekeza katika utafiti," alisema Erdogan.
‘Uwezo wa Uturuki kiteknolojia ulimwenguni’
Akiangazia malengo ya Uturuki, Erdogan amesema kuwa mkakati huo wa mwaka 2030 utakuwa ni chanzo cha maendeleo ya taifa ili kuhakikisha nchi hiyo inapambana na taasisi kubwa za kiteknolojia ulimwenguni.
"Tunachukua hatua madhubuti kuhakikisha kuwa Uturuki inajitegema," alisema Erdogan akiongeza. "Mkakati huu utaifanya Uturuki kuwa kitovu cha teknolojia, viwanda na ubunifu."