Waziri wa Ulinzi wa Urusi Andrey Belousov amefanya mazungumzo na mwenzake wa Jamhuri ya Congo, Luteni Jenerali Charles Richard Mondjo, kujadili ushirikiano katika masuala ya ulinzi ya mataifa hayo mawili.
Katika taarifa, wizara ya Ulinzi ilisema Belousov alisisitiza kuhusu uhusiano "wa kirafiki wa tangu jadi" kati ya Urusi na Jamhuri ya Congo, akisema nchi hizo mbili zimeanzisha mchakato wa kisheria kwa ajili ya ushirikiano wa kijeshi.
"Tunachukulia kwa uzito sana urafiki wetu wa tangu jadi wa ushirikiano kati ya nchi zetu. Kwa hali hii, ushirikiano wetu katika masuala ya kijeshi na masuala ya kiufundi ya kijeshi ndiyo yanayotuongoza katika uhusiano wa mataifa yetu mawili," alisema.
Pia alimshkuru Mondjo kwa kuhudhuria sherehe za kuadhimisha miaka 80 ya ushindi wa Sovieti katika vita vya pili vya dunia.
Mondjo, kwa upande wake, alitoa shukrani zake kwa kupata fursa ya kujadiliana masuala ya ushirikiano wa ulinzi kati ya mataifa yetu mawili.