Watu zaidi ya 100,000 wameyakimbia makazi yao nchini DRC ndani ya kipidi cha miezi mitano, Umoja wa Mataifa ulisema siku ya Ijumaa.
"Katika kipindi cha chini ya miezi mitatu, idaidi ya raia wa Congo wanaokimbilia nchi jirani imevuka 100,000," amesema msemaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR).
Machafuko yamekumba maeneo yenye utajiri wa madini nchini DRC, huku vikosi vya M23 vinavyoungwa mkono na Rwanda vikiendelea kudhibiti baadhi ya maeneo kadhaa mashariki mwa DRC.
Hatua hiyo imewalazimu majeshi ya serikali ya Congo kukimbia maeneo ya Kaskazini na Kusini mwa Kivu.
"Kulikuwa na wakimbizi wa ndani wapatao 400,000 katika eneo la Kivu Kaskazini, ," liliongeza shirika la UNHCR.
"Mashirika ya kibinadamu yanapata wakati mgumu kujenga makazi kutokana na masharti ya misaada kubadilika."