AFRIKA
1 dk kusoma
Tanzania yalitaka Bunge la Ulaya kuheshimu uhuru, sheria na maadili ya Taifa
Kauli hiyo ya Tanzania imekuja kufuatia mjadala uliofanyika katika Bunge la Ulaya kuhusu masuala ya ndani ya Tanzania.
Tanzania yalitaka Bunge la Ulaya kuheshimu uhuru, sheria na maadili ya Taifa
Tanzania imeonya kuwa Bunge la Ulaya halipaswi kutoa maamuzi yake kwa misingi ya taarifa zisizo kamili / Other
9 Mei 2025

Wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania imelitaka Bunge la Ulaya kuheshimu uhuru, sheria na maadili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikisisitiza kuwa nchi hiyo ni huru, ina Katiba yake na mfumo wa kisheria unaojitegemea.

Katika taarifa rasmi, wizara hiyo imesema kuwa maamuzi ya mahakama za Tanzania ni huru na hayapaswi kuingiliwa na taasisi za nje.

Aidha, imebainisha kuwa Tanzania inaheshimu uhuru wa kisiasa, uhuru wa vyombo vya habari, na tayari imepitisha sheria mpya ya uchaguzi mwezi Machi 2024, hatua iliyochangia kuanzishwa kwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.

Wizara hiyo pia imeonya kuwa Bunge la Ulaya halipaswi kutoa maamuzi yake kwa misingi ya taarifa zisizo kamili au zenye upendeleo, na kulihimiza bunge hilo kuheshimu mfumo wa kisheria na maadili ya Tanzania, sawa na jinsi Tanzania inavyoheshimu uhuru wa Bunge la Ulaya.

Kauli hiyo ya Tanzania imekuja kufuatia mjadala uliofanyika katika Bunge la Ulaya kuhusu masuala ya ndani ya Tanzania, hususan kesi zinazomkabili mwanasiasa Tundu Lissu, ambaye anakabiliwa na mashitaka kadhaa nchini humo.

CHANZO:TRT Afrika
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us