Utajiri wa Afrika: Siafu wakubwa wa kipekee
Utajiri wa Afrika: Siafu wakubwa wa kipekee
Siafu hawa wanapatikana hasa nchini Kenya, Tanzania na Ethiopia na wanaishi katika makundi makubwa ya zaidi ya siafu 5,000 hivi, umuhimu wao mkubwa ni katika ikolojia.
8 Mei 2025

Kuhukumiwa kwa vijana wanne, watatu wa nchi za kigeni na mahakama ya Kenya kwa sababu tu walipatikana wakijaribu kusafirisha siafu nje ya nchi, kuliwashangaza wengi. 

Vijana hao, wamehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja au faini ya dola 7000 kwa kosa la kujaribu kusafirisha wadudu hao kinyume cha sheria.

Wengi waliwaza na kuuliza iwapo ni siafu hawa wa kawaida au kuna wengine? Jibu hapa ni, siafu hao sio wa kawaida.

Ni aina ya kipekee inayopatikana barani Afrika tu.  Wanaitwa “Giant African Harvester Ants” kwa Kiingereza. 

Siafu hawa ndio wakubwa zaidi ya spishi zake na inaweza kukua hadi kufikia milimita 20 huku na malikia siafu akikuwa hadi kufikia milimita 25. 

Wanapatikana hasa Kenya, Tanzania na Ethiopia na wanaishi katika makundi makubwa ya siafu 5,000 hivi. Umuhimu wao ni tabia yao. 

Wao hula mbegu, ambazo wanakusanya na kuzihifadhi kwenye viota vyao, chini ya ardhi na hivyo kuchukua jukumu muhimu la kiikolojia kama wasambazaji wa mbegu na kuwa wahandisi wa udongo.

Wana uwezo wa kuwasiliana kupitia ishara za kemikali wanazotoa na kuacha harufu hivyo huwawezesha wenzao kufuata vyanzo vya chakula kwa ufanisi. 

Kwa wastani, siafu wa kawaida huishi kati ya mwaka 1 hadi 2, kulingana na ukubwa, wakati siafu malkia anaweza kuishi kwa miaka 27. 

TRT Global - Waliojaribu kutorosha siafu kupitia JKIA kuhukumiwa mwezi ujao

Washukiwa hao wanne wamekiri makosa yao wiki iliyopita baada ya mamlaka kuwakamata wakiwa na siafu 5,000.

🔗

Lakini kuna watu ambao wanawamezea mate kwa sababu tofauti na umuhimu wao kwa ikolojia. 

Katika nchi za bara la Ulaya na Asia, kuna soko kubwa la siafu hawa hasa kwa watu ambao wanapenda kuwatunza kama wadudu wa nyumbani.

Wakiwathamini kwa sababu ni wadudu nadra ambao sio kawaida kuhifadhiwa. Katika nchi hizi, kunaripotiwa ongezeko la maonyesho ya ufugaji wa siafu hawa, ambapo wanaowafuga hukutana ili kulinganisha maelezo ya makazi yao na aina ya siafu. 

Wengine wanasisimka kuwatazama kwa sababu ya ukubwa wao, rangi ya kipekee, tabia na jinsi wanavyokua. 

TRT Global - Jela kwa wasafirishaji wa siafu Kenya

Miongoni mwa wanne hao kuna raia wawili wa Ubelgiji ambao walipatikana na hatia kwa kujaribu kusafirisha siafu hao adimu nje ya nchi.

🔗

Siafu hawa wanauzwa kwa wingi mtandaoni, huku wafanyabiashara wakiwaorodhesha kama bidhaa "moto" sana. 

Kwa mfano, hapa mtandaoni tunaona wakiuzwa hadi dola 580, na bei itaongezeka kulingana na idadi ya siafu unayotaka kununua. Hii imesababisha kuibuka kwa wimbi la wasafairishaji haramu. 

Watu waliokamatwa Kenya kwa mfano walikuwa na siafu 5300, waliokadiriwa kuwa na thamani ya dola 9,200.

Mwaka wa 2013 watu watatu walikamtwa Kenya wakijaribu kusafirsha aina hiyo hiyo ya siafu waliokuwa na thamani ya dola $2,300 kwenda Ufaransa na China.


CHANZO:TRT Afrika and agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us