AFRIKA
2 dk kusoma
Makamu wa rais Sudan Kusini azuiliwa
Chama cha Makamu wa Rais wa kwanza Sudan Kusini kimesema walinzi wa kiongozi huyo walinyang'anywa silaha, na alifikishiwa hati ya kukamatwa kwa mashtaka ambayo hayakufahamika. Juhudi za kumhamisha kwa sasa zinafanywa," ilisema taarifa hiyo
Makamu wa rais Sudan Kusini azuiliwa
Makamu wa rais wa Sudan Kusini Riek Machar wamezuiliwa na maafisa wa serikali / AA
27 Machi 2025

Kufuatia taarifa ya usiku wa kuamkia leo ya kuzuiliwa kwa Makamu wa Kwanza wa Rais, Dkt. Riek Machar, ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, umetoa wito kwa wanachama wote kuwa makini na kuheshimu Makubaliano yaliyoimarishwa ya Amani.

"Usiku wa leo, viongozi wa nchi wana hiari ya kurejesha taifa kwenye hatari ya migogoro au kuipeleka nchi mbele katika misingi ya amani, utulivu na demokrasia kwa kuzingatia makubaliano yaliyofikiwa mwaka 2018 walipotia saini na kujitolea kutekeleza Mkataba ulioimarishwa wa Amani," alisema Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu na Mkuu wa UNMISS, Nicholas Haysom.

Katika taarifa, chama cha Machar cha SPLM-IO kimelaani "ukiukaji wa wazi wa Katiba na Mkataba wa Amani Ulioimarishwa," ambao ulimaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vya 2013-2018 kati ya vikosi vinavyomtii Machar kwa upande mmoja na Rais Salva Kiir kwa upande mwingine.

TRT Global - Naibu Rais wa Sudan Kusini ataka majeshi ya Uganda kuondoka

Uganda ilisema kuwa ilituma wanajeshi wake nchini Sudan Kusini mapema mwezi huu kufuatia ombi la serikali baada ya kuvunjika kwa uhusiano kati ya Machar na Rais Salva Kiir.

🔗

"Walinzi wake walinyang'anywa silaha, na alifikishiwa hati ya kukamatwa kwa mashtaka ambayo hayakufahamika. Kwa sasa mipnago ya kumhamisha inaendelea," ilisema taarifa hiyo.

Nchi za ndani ya Afrika na mataifa ya nje zinahofia kwamba vita vya wenyewe kwa wenyewe vinaweza kuzuka tena nchini Sudan Kusini kufuatia majuma kadhaa ya mvutano unaongezeka ambao ulitokana na mapigano kati ya wanajeshi wa serikali na wapiganaji ambao kihistoria wamekuwa karibu na vikosi vya Machar.

Katika kukabiliana na mapigano tangu mwishoni mwa mwezi Februari katika jimbo la Upper Nile kaskazini mashariki, serikali ya Kiir imewakamata maafisa kadhaa wa chama cha Machar, akiwemo waziri wa mafuta na naibu mkuu wa majeshi.

Mapema siku ya Jumatano, Umoja wa Mataifa ulitoa taarifa ya mapigano katika muda wa saa 24 zilizopita kati ya vikosi vinavyomtii Kiir na Machar nje ya mji mkuu Juba.

"Kwenda kinyume na makubaliano ya amani kunaweka kwenye ati ati mafanikio yaliyopatikana katika miaka saba iliyopita na kuna hatari ya kuirejesha nchi katika vita. Hii sio tu itaharibu Sudan Kusini lakini pia itaathiri eneo zima," Haysom aliongeza.

UNMISS imetowa wito kwa wadau wote wa makubaliano ya amani kuacha mara moja uhasama na kushiriki katika mazungumzo yanayozingatia maslahi ya wananchi wa Sudan Kusini wakati huu muhimu kwa taifa hilo jipya zaidi duniani.

CHANZO:TRT Afrika
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us