AFRIKA
1 dk kusoma
Tanzania kuvaana na Morocco ikisaka tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia 2026
Mchezo huo umepangwa kufanyika katika uwanja wa Honneur jijini Oujda nchini Morocco, Machi 26, 2025.
Tanzania kuvaana na Morocco ikisaka tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia 2026
Kikosi cha ‘Taifa Stars’ kinatarajiwa kutangazwa na Kocha Mkuu wa timu hiyo Hemed “Morocco” Suleiman, Machi 14, 2025./Picha: @TaifaStars_ / Others
14 Machi 2025

Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, itakuwa na kibarua kigumu pale itakapokuwa mgeni wa ‘Simba kutoka milima ya Atlas’ kutoka Morocco katika mchezo wa kuwania nafasi ya kushiriki Fainali za Kombe la Dunia kwa mwaka 2026.

Mchezo huo umepangwa kufanyika katika uwanja wa Honneur jijini Oujda nchini Machi 26, 2025.

‘Taifa Stars’ inashika nafasi ya tatu katika msimamo wa kundi E, ikiwa na alama 6 baada ya michezo mitatu, huku viongozi wa kundi hilo, Morocco wakiwa na rekodi nzuri ya alama 9 baada ya michezo mitatu.

Ikiwa na alama 6, Niger inashika nafasi ya pili, wakiwa na faida ya mabao ukilinganisha na Tanzania.

Zambia iko nafasi ya nne ikiwa na alama 3 baada ya michezo minne, huku Congo Brazzaville, ambayo ilisimamishwa na FIFA iko katika nafasi ya tano.

Kikosi cha ‘Taifa Stars’ kinatarajiwa kutangazwa na Kocha Mkuu wa timu hiyo Hemed “Morocco” Suleiman, Machi 14, 2025.

Tanzania haijawahi kushiriki fainali za Kombe la Dunia katika historia yake.

Fainali hizo, ambazo zinaandaliwa kwa pamoja na Marekani, Mexico na Canada zinatarajiwa kufanyika kuanzia Juni 11, 2026 hadi Julai 19, 2026.

CHANZO:Wengine
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us