AFRIKA
2 dk kusoma
Mashambulizi ya anga Darfur yaua 14 kutoka familia moja
Watu hao wa familia moja wameuliwa baada ya kushambuliwa kwa kambi ya Abu Shouk na vikosi vya RSF Ijumaa jioni, vikosi vya uokoaji vimesema.
Mashambulizi ya anga Darfur yaua 14 kutoka familia moja
Wanawake wakimbizi wakiwa katika kambi ya Abu Shouk, Darfur. / Getty
10 Mei 2025

Takriban watu 14 kutoka familia moja wameuliwa katika shambulizi la anga lililofanyika katika kambi ya waliokosa makazi. Mashambulizi hayo yamefanyika katika eneo lenye mapigano la Darfur nchini Sudan, kikosi cha waokoaji kimesema Jumamosi, huku kikilaumu wapiganaji wa RSF.

Kambi ya Abu Shouk “ililengwa kwa mabomu na vikosi vya RSF Ijumaa jioni,” kimesema kikosi cha kujitolea cha misaada, ambacho pia kimesema kuna waliojeruhiwa.

“Raia 14 wa Sudan, kutoka familia moja, wameuawa, na wengine kadhaa kujeruhiwa,” imesema taarifa iliyotolewa.

Kambi ya El-Fasher, mji wa mwisho Darfur ambao bado hauko chini ya himaya ya RSF, inakabiliwa na ukame, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.

Imeshambuliwa mara kadhaa

Kambi hiyo inakaliwa na maelfu ya watu ambao wamekimbia mapigano Darfur katika nchi ya tatu kwa ukubwa Afrika.

RSF ambayo inapigana na jeshi la nchi hiyo, imeshambulia kambi hiyo mara kadhaa katika wiki za hivi karibuni.

Abu Shouk iko karibu na kambi ya Zamzam, ambayo ilichukuliwa na RSF mwezi Aprili baada ya mapambano makali ambayo yameiacha ikiwa tupu.

Umoja wa Mataifa unasema takriban watu nusu milioni walikua wamepata hifadhi katika eneo hilo.

Janga la kibinadamu

Vita vilianza kati ya jeshi cha Abdel Fattah al-Burhan na aliyekuwa makamu wake, mkuu wa RSF Mohamed Hamdan Daglo, wote wakitaka madaraka. Umoja wa Mataifa unasema vita hivyo mpaka sasa vimesababisha janga kubwa la kibinadamu.

Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us