MICHEZO
1 dk kusoma
Rwanda, Nigeria katika mechi ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia
Huku mchakato wa kuwania kufuzu kwa Kombe la Dunia 2026 ukiendelea, Nigeria wako mjini Kigali kumenyana na wenyeji Rwanda, wakitarajia kufufua matumaini ya kufuzu kwa michuano hiyo.
Rwanda, Nigeria katika mechi ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia
Timu ya taifa ya Nigeria ikicheza katika moja ya mechi zao 2024. Picha: Getty / Getty
21 Machi 2025

Nigeria imecheza mechi nne kufikia sasa lakini hawajapata ushindi wowote. Super Eagles ambao watatarajia kuwa wataondoka na alama tatu watakapokuwa Amahoro usiku wa Ijumaa wako katika nafasi ya tano kati ya timu sita wakiwa na alama 3 pekee.

Vijana wa Rwanda, Amavubi wako nafasi ya pili kwenye kundi C wakiwa na alama 7 baada ya kucheza mechi nne. Wanaoongoza kundi hilo ni Benin wenye alama 8, baada ya kukamilisha mechi tano.

Amavubi walifungwa na Benin 1-0 mwaka uliopita mwezi Juni lakini wakafanikiwa kupata ushindi dhidi ya Lesotho.

Rwanda wana kocha mpya Adel Amrouche ambaye analenga kuipeleka timu hiyo kwenye mashindano ya Kombe la Dunia. Amavubi haijawahi kushiriki kwenye michuano hiyo na wataichukua mechi hii dhidi ya Super Eagles kama fursa ya kurejea juu ya msimamo wa jedwali katika kundi hilo.

Nigeria ilimteua kocha mwenye uraia pacha wa Ufaransa na Mali Eric Chelle mwezi Januari, Ana jukumu muhimu la kurejesha mafanikio ya timu hiyo na kuwafunga midomo wakosoaji.

Super Eagles ikipata ushindi mjini Kigali, watakuwa wamefufua matumaini yao ya kuelekea kwenye kombe la Dunia 2026.

Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us