17 Machi 2025
Kikundi cha waasi wa AFC/M23 kimetangaza kutoshiriki mazungumzo ya amani, wakiituhumu serikali ya Rais Felix Tshisekedi kwa kuendeleza vita.
Katika taarifa yake iliyotolewa Februari 17, 2025, kundi la M23 limeituhumu serikali ya DRC kwa kuendeleza mashambulizi ya ardhini kwa kutumia ndege za kivita.
Taarifa hiyo inakuja muda mchache baada ya AFC/M23 kusema kuwa itatuma wawakilishi nchini Angola kwa ajili ya mazungumzo ya amani ambayo yamepangwa kufanyika Machi 18.
Mapema Machi 17, msemaji wa M23 Lawrence Kanyuka alisema kuwa wawakilishi wao wangesafiri kuelekea Luanda kwa ajili ya mazungumzo hayo.
Mazungumzo hayo yanaratibiwa na Rais wa Angola João Lourenço, baada ya kukutana na Rais wa DRC Felix Tshisekedi.