ULIMWENGU
1 dk kusoma
Vatican: Papa Francis kutoa baraka za Pasaka
Papa Francis, mwenye umri wa miaka 88, aliruhusiwa kutoka hospitali ya Gemelli, Jumapili iliyopita, baada ya kuwa amelazwa tangu Februari 14, 2025, akisumbuliwa na maradhi ya homa ya mapafu.
Vatican: Papa Francis kutoa baraka za Pasaka
Papa Francis, mwenye umri wa miaka 88, aliruhusiwa kutoka hospitali ya Gemelli, Jumapili iliyopita, baada ya kuwa amelazwa kutoka tangu Februari 14, 2025, akisumbuliwa na maradhi ya homa ya mapafu./Picha: Getty / Others
27 Machi 2025

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis amenuia kutoa baraka za siku ya Pasaka, licha ya changamoto ya afya inayomkabili.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na Vatican siku ya Alhamisi, Papa Francis ambaye anakabiliwa na maradhi ya homa ya mapafu, ameweka nia ya kutoa baraka za sikukuu ya Pasaka, ambayo itaadhimishwa ulimwenguni kote, Jumapili ya Aprili 20, 2025.

Hata hivyo, taarifa ya Vatican haikuweza wazi iwapo Baba Mtafatifu huyo ataweza kuadhimisha ibada ya misa siku hiyo.

TRT Global - Papa Francis hakuhitaji msaada wa Oksijeni wakati wa kulala, yasema Vatican

Kulingana na madaktari wa hospitali ya Gemelli, afya ya Papa Francis inaendelea kuimarika baada ya kupata shida ya kupumua, hali iliyoibua hofu kuhusu afya yake.

🔗

Papa Francis, mwenye umri wa miaka 88, aliruhusiwa kutoka hospitali ya Gemelli, Jumapili iliyopita, baada ya kuwa amelazwa kutoka tangu Februari 14, 2025, akisumbuliwa na maradhi ya homa ya mapafu.

Hata hivyo, hali ya afya ya Baba Mtakatifu huyo imeibua maswali mengi kuhusu iwapo ataweza kuadhimisha ibada ya sikukuu ya Pasaka, ambapo Wakristu wote ulimwenguni huadhimisha siku ya kufufuka kwa Yesu Kristo.

Kipindi cha Pasaka, ni ukamilisho wa siku 40 za Kwaresima, ambazo Wakristu hutumia kufunga, kufanya toba, kusali na kusaidia masikini.

TRT Global - Hii ni Kwaresima

Ikiwa imetoholewa kutoka neno la Kilatini ‘Quadragesima’ lenye maana ya 40, kipindi cha Kwaresima ni siku 40 za hija ya kiroho.

🔗

Kila sikukuu ya Pasaka, Baba Mtakatifu hutoa baraka kwa ulimwengu, yaani "Urbi et Orbi", kwa lugha ya Kilatini.

Baraka hiyo hutolewa kwenye dirisha la Kanisa la Mtakatifu Petro, jijini Roma.

CHANZO:AFP
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us