MICHEZO
1 dk kusoma
Libya yamteua Aliou Cisse mshindi wa AFCON kuwa Kocha Mkuu wa timu ya taifa
Aliou Cisse anaheshimiwa kama mmoja wa makocha wenye uzoefu mkubwa barani Afrika
Libya yamteua Aliou Cisse mshindi wa AFCON kuwa Kocha Mkuu wa timu ya taifa
Kocha Aliou Cisse alizaliwa Senegal mwaka 1976. / AFP
12 Machi 2025

Shirikisho la soka la Libya limemteuwa kocha aliyeshinda mashindano ya kombe la mataifa ya bara Afrika AFCON Aliou Cisse kuwa kocha mkuu wa timu yao ya taifa.

Cisse,anayeaminika kuwa mmoja wa makocha wenye uzoefu mkubwa barani na mshindi wa AFCON na Senegal 2022,amesaini mkataba na Libya wa hadi 2027,shirikisho hilo limesema kwenye taarifa siku ya Jumanne.

"Tunamkaribisha kocha bora kabisa barani Afrika,"taarifa hiyo ilisema,bila kutoa maelezo zaidi kuhusu mkataba mpya wa Cisse au kitita atakacholipwa.Anachukua nafasi ya Nasser Al-Hadhiri,ambaye aliteuliwa Septemba 2024.

Shirikisho hilo linasema Cisse,48, atatangazwa rasmi katika mkutano na waandishi wa habari Tarehe 13 Machi mjini Tripoli.Libya haikufuzu kwa AFCON inayotarajiwa kufanyika nchini Morocco mwishoni mwa mwaka huu.

Hata hivyo,wako kwenye nafasi ya pili katika kundi lao la kuania kufuzu kwa Kombe la Dunia,na watacheza dhidi ya Angola baadaye mwezi huu.

Tazama:

CHANZO:AFP
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us