ULIMWENGU
1 dk kusoma
Papa Francis aacha kupumua kwa kutumia oksijeni, yasema Vatican.
Kwa mujibu wa Vatican, Papa Francis ameacha kupumua kwa msaada wa mashine za oksijeni, ikiongeza kuwa hali yake ya upumuaji ikizidi kuimarika.
Papa Francis aacha kupumua kwa kutumia oksijeni, yasema Vatican.
Baba Mtakatifu huyo amekuwa hospitalini hapo tangu Februari 14, akisumbuliwa na maradhi ya homa ya mapafu./Picha: Getty / Others
19 Machi 2025

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis ameacha kupumua kwa msaada wa hewa ya oksijeni, taarifa iliyotolewa na Vatican siku ya Jumatano, imesema.

Kulingana na Vatican, afya ya kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 88 inazidi kuimarika, akiwa ametimiza zaidi ya mwezi mmoja ndani ya hospitali ya Gemelli.

Baba Mtakatifu huyo amekuwa hospitalini hapo tangu Februari 14, akisumbuliwa na maradhi ya homa ya mapafu.

"Afya ya Baba Mtakatifu inazidi kuimarika,” ilisema Vatican kupitia jarida lake lake la afya.

Kwa mujibu wa Vatican, Papa Francis ameacha kupumua kwa msaada wa mashine za oksijeni, ikiongeza kuwa hali yake ya upumuaji ikizidi kuimarika.

CHANZO:AFP
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us