ULIMWENGU
1 dk kusoma
Moto katika kituo cha umeme, wasababisha kufungwa kwa Uwanja wa Ndege wa Heathrow
Uwanja wa ndege wa London umefungwa mpaka saa sita usiku wa kuamkia Machi 21 kutokana na umeme kuzimwa
Moto katika kituo cha umeme, wasababisha kufungwa kwa Uwanja wa Ndege wa Heathrow
Zaidi ya safari za ndege 1,350 zimesimamishwa katika uwanja wa ndege wa Heathrow f / Reuters
21 Machi 2025

Uwanja wa Ndege wa Uingereza wa Heathrow mapema Ijumaa umesema kwamba umelazimika kufungwa kufuatia ajali ya moto katika kituo cha umeme kinachotumika kusambaza nishati hiyo.

“Ili kuwa na usalama kwa abiria wetu na wenzetu, Heathrow itafungwa mpaka saa tano na dakika 59 usiku wa kuamkia Machi 21,” taarifa hiyo imetolewa katika mtandao wa X.

Abiria wameshauriwa kutosafiri katika uwanja huo na kuwasiliana na mashirika yao ya ndege kwa taarifa zaidi.

“Tunaomba radhi kwa usumbufu,” imeongeza kusema taarifa hiyo. Heathrow ni kati ya viwanja vikubwa vya ndege duniani, huku mamilioni ya abiria wakiutumia uwanja huo kwa mwaka. Kufungwa kwa uwanja huo kutaathiri safari za ndege na mipango ya wasafiri.

CHANZO:Anadolu Agency
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us