Mwanariadha wa Kenya Sabastian Sawe alicheza vyema na kushinda katika mbio zilizowakusanya nyota wakubwa duniani za London marathon katika muda wa saa 2 dakika 02 dakika 27 sek Jumapili.
Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 29, ambaye alishinda mbio za marathon za Valencia Desemba mwaka jana, alimaliza mkondo wa mwisho peke yake kwenye jua kali mbele ya bingwa wa rekodi ya dunia ya nusu marathon wa Uganda Jacob Kiplimo.
Bingwa mtetezi Alexander Mutiso Munyao, pia Mkenya, alimshinda Abdi Nageeye katika nafasi ya tatu kujipatia nafasi jukwaani huku bingwa mara nne Eliud Kipchoge akimaliza wa sita.
Katika hatua ya nusu ya mbio hizo kundi lililoongoza, lililojumuisha Kipchoge, bingwa wa Olimpiki Tamirat Tola na Kiplimo, walitoka nje ya kasi ya rekodi ya dunia saa 1:01:30.
Kasi ya maamuzi
Kipchoge, hata hivyo, aliachwa nyuma huku wakimbiaji wakikaribia dakika 90.
Ilikuwa ni kwenye kituo cha kunywa maji muda mfupi baada ambapo Sawe alifanya maamuzi madhubuti. Tofauti na wengine, hakunywa kinywaji na ilimsaidia kupata hatua kadhaa mbele yao.
Kufumba na kufumbua Kiplimo alijikuta nyuma ya kundi, lakini kijana huyo mwenye umri wa miaka 24 alipambana kwa chote alicho nacho.
Sawe, hata hivyo, hakuwa na wasiwasi tangu wakati huo na kuendelea, alionekana freshi na mtulivu akivuka utepe kwenye kivuli cha Buckingham Palace.