AFRIKA
1 dk kusoma
Kiongozi wa Sudan al-Burhan amteua Al-Haj kama waziri mkuu wa serikali ya mpito
Al-Burhan pia ameidhinisha uteuzi wa mawaziri wengine wapya
Kiongozi wa Sudan al-Burhan amteua Al-Haj kama waziri mkuu wa serikali ya mpito
Rais wa Baraza la Mpito la Sudan Abdel-Fattah Al-Burhan
1 Mei 2025

Mwenyekiti wa Baraza la Mpito linalotawala nchini Sudan Jenerali Abdel Fattah al-Burhan siku ya Jumatano amemteua Balozi Dafallah al-Haj Ali kuwa waziri wa masuala ya baraza na waziri mkuu wa serikali ya mpito.

Al-Haj ni balozi wa Sudan nchini Saudi Arabia na amekuwa katika Wizara ya Mambo ya Nje tangu 1980.

Amewahi kuhudumu kama balozi nchini Pakistan,Vatican na Ufaransa, na pia kama mwakilishi katika Jumuiya ya Ushirikiano wa nchi za Kiislamu (OIC) na Umoja wa Mataifa.

Burhan pia aliidhinisha uamuzi wa baraza la mawaziri la kumteua balozi Omar Mohamed Ahmed Siddig kama waziri wa mambo ya nje na Dkt. al-Tahami al-Zein Hajar Mohamed kama waziri wa elimu.

Serikali ya mpito ilianzishwa na Burhan mwezi Aprili 2019, kufuatia mapinduzi ya kijeshi yaliyomuondoa madarakani aliyekuwa rais wakati huo Omar al-Bashir. Baraza la mpito liliundwa mwezi Agosti mwaka huo na Baraza la sasa likashikilia hatamu kuanzia Novemba 2021.

Tangu 15 April 2023, vikosi vya wapiganji wa RSF vimekuwa vikikabiliana na jeshi la Sudan kwa lengo la kuchukua udhibiti wa nchi.

Mapigano hayo yamesababisha mauaji ya maelfu ya watu, na moja ya hali mbaya zaidi kwa watu duniani.​​​​​​​

CHANZO:AA
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us