Na Na'eem Jeenah
Balozi Ebrahim Rasool na mimi tumekuwa tukifahamiana kwa muda mrefu. Mwanzoni mwa miaka 80, sote tulikuwa wanaharakati dhidi ya utawala wa kibaguzi.
Siku ya Ijumaa, nilikuwa na mkutano kwa njia ya mtandao kuangazia sera za Marekani zinamaanisha nini au zitatoa muelekeo gani kwa bara la Afrika kwa jumla na hususan kwa Afrika Kusini.
Mada tuliyoamua kuijadili ni uongozi mpya wa Marekani na athari yake kwa bara la Afrika, kanda ya Kusini mwa Afrika na bila shaka Afrika Kusini.
Ambassador Rasool alikuwa ndiye mgeni rasmi.
Amekuwa Marekani kwa takriban miezi miwili, na kabla ya hapo, alikuwa huko kwa miaka minne kama balozi wa Afrika Kusini nchini Marekani.
Rasool ana ufahamu mzuri wa siasa za Marekani, na ni raia wa Afrika Kusini, na bila shaka anafahamu masuala ya kupewa kipaumbele katika uhusiano Marekani na Afrika Kusini.
Wazungumzaji wengine wanne walialikwa kuzungumzia masuala kama hayo katika mkutano huo wa saa mbili.
Madai ya uwongo ya Trump kwa Afrika Kusini
Katika hotuba yake ya ufunguzi, Balozi Rasool alieleza umuhimu wa uhusiano kati ya Marekani na Afrika Kusini.
Anaamini Afrika Kusini inatakiwa kuchukuwa hatua kali dhidi ya Marekani licha ya agizo la Rais Donald Trump alilotia saini dhidi ya Afrika Kusini.
Kwa upande wa biashara, pia alieleza kuwa, 80% ya kile China inaagiza kama malighafi kutoka Afrika Kusini, Marekani inaagiza 70% ya bidhaa zilizotengenezwa kutoka Afrika Kusini
Kesi ya Afrika Kusini dhidi ya Israeli
Alikuwa anazungumzia kuhusu sheria ya ardhi ya Afrika Kusini, ambayo ilitiwa saini na Rais Cyril Ramaphosa Januari mwaka huu lakini bado haijatekelezwa. Kwa hiyo, hakuna mali ya mtu ambayo imechukuliwa. Hii ndiyo ilikuwa sababu yake ya kwanza kwenye agizo la rais.
Sababu ya pili ilikuwa kuhusu kesi ya Afrika Kusini dhidi ya Israeli katika mahakama ya ICJ, ambapo Afrika Kusini inaituhumu Israeli kwa mauaji ya halaiki huko Gaza.
Kwa hiyo, katika kujibu swali hilo balozi Rasool aliwaelezea Waafrika Kusini namna serikali mpya ya Marekani itakavyofanya kazi.
Alieleza kuwa katika miaka michache ijayo, Marekani itakuwa na wazungu 48% pekee na uongozi wa Trump unajiandaa kutetea tabaka hilo la wazungu.
Aliongeza masuala ya nyumbani, serikali ya Trump imeangazia suala hilo duniani kote.
Kwa mfano, Makamu wa Rais JD Vance anasifia mambo ya kibaguzi, chama kinachopinga wahamiaji nchini Ujerumani cha AfD na mwanasiasa wa mrengo wa kulia nchini Uingereza Nigel Farage.
Serikali ya Trump ina mtazamo kama huo kwa wazungu wa Afrika Kusini, ni kama ambaye utawala wa Trump ndiyo mtetezi wa wazungu wote kote duniani.
Namna Marekani ilivyojibu kwa ukali
Balozi, alikuwa anajaribu kufafanua kile ambacho tunaona sasa hivi tabaka la wazungu.
Na ndiyo hilo pekee ambalo lilionekana na mtandao wa kundi la Marekani la mrengo wa kulia, Breitbart na matokeo yake kusahau kila alichokizungumza kwenye mkutano huo.
Makala ya Breitbart yaliyoandikwa na Joel Pollak, Mmarekani mhafidhina aliyezaliwa Afrika Kusini, ambaye anatafuta nafasi ya kuwa balozi wa Marekani nchini Afrika Kusini!
Pollak, alichukuwa sehemu hiyo kwa makusudi kuhusu mabadiliko ya watu wa Marekani na serikali ya Trump kujiandaa kutetea wazungu.
Na ndiyo makala ambayo Waziri wa Mambo ya Nje Marco Rubio alisoma na kutumia kama msingi wa kumtimua balozi wa Afrika Kusini Ebrahim Rassool nchini Marekani!
Afrika Kusini haina uadui ‘dhidi ya Marekani’
Pengine hatua ya kwanza ingekuwa kutatuliwa kidiplomasia au kwa mawaziri wa nchi hizo mbili wa mambo ya nje kujadili kile alichofanya balozi huyo.
Badala yake, wakachukua hatua kali, hatua ambayo hutumika kwa mabalozi ambao wanajihusisha na vitendo vya kijasusi.
Kwa hakika, sote tulishtushwa na hatua hiyo, kwamba Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani amechukuwa hatua hizo kali sana dhidi ya balozi.
Balozi alikuwa muwazi na mkweli, lakini hatukudhani kwamba alisema lolote kufanya hatua hiyo kuchukuliwa.
Balozi Rasool amewahi kuwa balozi nchini Marekani.
Sidhani kama mtu yeyote ambaye ameamiliana naye angeamini kuwa yeye ni adui wa Marekani.
Cha kushangaza, alishutumiwa kwa kupendelea Marekani baada ya mkutano huo, hasa kwa kuwaambia Waafrika Kusini kujizuia na kutoa kauli mbaya dhidi ya agizo la rais Trump. Siyo adui wa Marekani.
Rais wetu hawezi kumteua mtu kwa nafasi ya ubalozi ambaye angeamini atakuwa dhidi ya Marekani.
Yote haya ya kupangwa yanatokana na Afrika Kusini kuipeleka Israeli katika mahakama ya ICJ.
Kuna masuala mawili hapa:
Kwanza ni nia ya serikali ya Trump kuilinda na kuitetea Israeli kwa vyovyote vile.
Hakuna kurudi nyuma katika kesi ya mauaji ya halaiki ICJ
Kesi ya Afrika Kusini dhidi ya Israeli katika mahakama ya ICC inaiweka sehemu mbaya na Marekani.
Pili, utawala wa Trump imeliweka wazi kuwa hauheshimu taasisi za kimataifa au sheria za kimataifa. Kwa kifupi, mtazamo wake, sheria isiyo rasmi ndiyo itatawala masuala ya kimataifa.
Kuhusu ICJ, msimamo wa Afrika Kusini uko wazi kuwa – watazingatia sheria ya kimataifa kama sehemu ya jumuiya ya kimataifa, hatuwezi kukubali ukiukwaji wa sheria za kimataifa wakati Israeli inaendelea kufanya hivyo Gaza.
Afrika Kusini haitorudi nyuma kwa hili. Serikali ya Afrika Kusini, pia inaamini kuwa tunawajibika kikatiba, kuhakikisha kuwa haki inapatikana na haki za binadamu zinazingaiwa kote duniani, na hilo ndilo tunalolifanya.
Afrika Kusini haina nia ya kugombana na Marekani. Nia ni kushughulikia masuala kidiplomasia jambo ambalo Rais Cyril Ramaphosa alieleza katika hotuba yake kwa taifa aliposisitiza kuwa nchi yake haitoburuzwa, kwamba tutafanya shughuli kimataifa kwa njia ya heshima na uadilifu.
Mwandishi, Na'eem Jeenah, ni Mtafiti Mwandamizi katika Taasisi ya Mapungubwe (MISTRA).
Kanusho: Maoni ya mwandishi hayaakisi maoni, mitazamo na sera za uhariri za TRT Afrika.